PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

KOREA KASKAZINI imesisitiza msimamo wake kuwa suala la raia wa Japani waliotekwa na nchi hiyo limetatuliwa.

Taasisi ya utafiti wa masomo ya Japani ya Wizara ya Mambo ya nje ya Korea Kaskazini ilitoa maoni hayo kwenye mtandao wa Wizara hiyo.

Maoni hayo yalitolewa huku Waziri Mkuu wa Japani Suga Yoshihide akikutana na familia za mateka siku hiyo hiyo kwa mara ya kwanza tangu alipoingia madarakani mapema mwezi huu.

Korea Kaskazini ilimshutumu mtangulizi wa Suga, Abe Shinzo, kwa kuendeleza sera ya kuchochea uhasama ikilinganishwa na watangulizi wake wote iliyolenga kuitenga na kuivuruga Korea Kaskazini kisiasa na kiuchumi.

Taarifa hiyo iliikosoa Serikali ya Suga kwa kufanya matukio yasiyokuwa ya kawaida ya kuomba hapa na pale ili kupata suluhisho la suala la mateka huku akiiga jaribio la Abe.

Suga aliziambia familia za mateka wakati wa mkutano huo kuwa ataendeleza juhudi na kutumia kila fursa kung’amua suala la mateka.