MIAKA miwili iliyopita, kampuni inayotengeneza simu za mkononi ya Samsung, ilisitisha mauzo ya simu mpya kwa wakati huo, Galaxy Note 7, baada ya malalamiko mengi ya wateja.

Watumiaji wa simu hizo waliilalamikia kampuni hiyo kwa kile walichokieleza kwamba betri za simu hiyo zinaripuka.

Samsung baada ya kupokea malalamiko hayo ililamika kufanua utafiti, ili jiridhisha dhidi ya madai ya wateja ambapo walibaini kuwa kasoro iliopo katika betri za simu hizo.

Simu hizo zilikuwa zinatumia betri ya Lithium-ion, ambayo hushika chaji haraka ni hatari sana kunapotokea kasoro kwa sababu husababisha moto.

Mtaalam mmoja ameiambia kampuni hiyo kutafuta madini mbadala ya lithium. ”Nadhani tunafaa kuwa na wasiwasi na kutafuta betri zilizo salama,”alisema mtaalam wa kuhifadhi nishati Profesa Clare Grey kutoka chuo kikuu cha Cambridge.

Hata hivyo Profesa Grey aliwaeleza wateja wa simu za Samsung hatokuwa na hofu.

Hadi Samsung ilipofanya utafiti huo, kulikuwa na matukio 35 ya simu za Galaxy Note 7 kushika moto duniani baada ya mauzo ya takriban simu milioni 2.5.

Betri za Lithium zinazotumika na Samsung hutumika sana katika viwanda vya kiteknolojia, lakini ni nini inachozifanya kuwa hatari?

Ni muhimu kujua vile zinavyofanya kazi. Betri hizo huwa na Cathode, Anode na Lithium.

Cathode na Anode huwa zimetawanywa na maji maji yanayoitwa elektrolait pamoja na kifaa kilicho na mashimo madogo kwa jina kitawanyishi.

Lithium hupitia kitawanyishi hicho ndani ya majimaji hayo, iwapo betri inapata chaji haraka na kupata joto, Lithium huzunguka katika Anode ambayo husababisha moto.

Kwa kawaida kuna eneo linalodhibiti chaji inayoingia katika betri hiyo, alisema Profesa Grey.

Betri huwekewa muda ili zisiweze kupata chaji kwa haraka. Hii ndio maana huchukua mda mrefu mtu anapochaji betri.

Lakini betri huanza kutoa ishara za kufura kabla ya kufeli kabisa kwa sababu seli zilizo ndani yake hufura na kupasuka lakini kufura huko hakutokei mara kwa mara.

Na iwapo haitafura utahisi joto lisilo la kawaida katika simu, lakini ukweli ni kwamba simu zetu huongeza joto wakati zinapotumika.

Hata hivyo kampuni hiyo inasema kuwa unapohisi betri yako imeanza kuwa na joto itoe na ununue nyengine.