HAPANA shaka yoyote binaadamu ana uhusiano mkubwa na wanyama. Hii inatokana nakwamba nadharia za kibailojia zinamtaja mwanadamu naye ni manyama.
Hata hivyo, utofauti baina ya binaadamu na mnyama ni mmoja tu nao ni uwezo mkubwa wa kutumia akili alizopewa na muumba wake tofauti na mnyama mwenye akili za kimaumbile.
Wanyama karibu wa aina zote hapa ulimwneguni wana sifa walizonazo viumbe wenye kuishi, sifa ambao mwanadamu kwa sababu naye ana ishi sifa hizo anazo.
Kumekuwa na uhusiano mkubwa katika maisha baina ya mwanadamu na wanyama, kiasi kwamba wapo baadhi ya wanyama mwanadamu anaishi nao nyumba moja na kuwapa mtunzo mzuri.
Mahusiano ya mwanadamu na wanyama pia yamefikia hatua ambayo hapo wali si rahisi kama ingedhaniwa itatokea. Kwa mfano mwadamau kwa kutumia akili anaweza kuishi na wanyama wakali basi na kutokea kwa madhara yoyote.
Mifano ipo mingi tunayoweza kuina, wapo nyoka hatari ambao wakimgonga mwanadamu katika mwili wake anaweza kupoteza maisha, mamba ambaye ukigusa mwili wa binadamu ameukata pande lakini mwanadamu anafuga.
Mwanadamu wakati mwengine huishi na mnyama akimpatia matunzo stahiki kwa kutegemea kuwa sehemu yake muhimu ya kupata chakula. Kwa bahati mbaya sana wanadamu hivi sasa wamekuwa akila kila aina ya wanyama.
Zipo baadhi ya jamii hapa duniani zinakula mbwa, paka, nyoka huku wakisifia kuwa nyama za wanyama hao ni tamu za zina virutubisho vingi vinavyoweza kujenga mwili wa binaadamu.
Kama lipo jambo la kuliangalia sana juu ya mahusiano ya binadaamu na wanyama ni kuwepo maambukizo ya maradhi ambayo mara nyingi hutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.
Kiukweli kabisa wanyama wamekuwa chanzo cha kumsababishia maradhi hatari mwanadamu yanayotokana na ama vurusi au bektiria. Tukianzia kwenye ebola, kichaa cha mbwa mafua ya nguruwe, mafua ya kuku, na hata maradhi ya ‘corona’ yaliyobuka huko nchini China.
Suali la kujiuliza wanyama wanawezaje kuwafanya watu waumwe? Kwa miaka zaidi ya 50, maambukizi ya magonjwa yamekuwa yakitoka kwa wanyama kwenda kwa binaadamu.
Mnamo mwaka 1980, kulibuka janga la virusi vya UKIMWI ambavyo vinadaiwa kuwa vilitokea kwa sokwe, mwaka 2004 mpaka 2007 mafua makali ya ndege na nguruwe pia walidaiwa kusababisha mafua makali ya Swine mwaka 2009.
Vilevile ilibainika kuwa maambukizi ya SARS yalitokana na popo huku ebola pia ikidaiwa kusababishwa na popo.
Binadamu wamekuwa wakipata magonjwa kutoka kwa wanyama, haswa maambukizi ya magonjwa ya hivi karibuni yanaelezwa kuwa yametokea kwa wanyama pori.
Lakini mabadiliko ya mazingira yanaongeza kasi ya maambukizi ya aina hiyo kutokea, huku ongezeko la watu wanaoishi mjini na kusafiri mataifa mbalimbali wakati ugonjwa huo umeanza unafanya maambukizi yasambae kwa kasi zaidi.
Kwa kawaida virusi vinavyoweza kumsababishia maradhi mwanadamu vinaweza kutoka kwa urahisi kutoka kwa wanyama hadi kwa binaadamu. Urahisi huu unategema mahusiano baina binadamu na wanyama.
Wanyama wengi huwa wana bakteria hatari na virusi ambavyo vinaweza kusababisha magonjwa, ambapo mzunguko wa virusi huwa unategemea nani ambaye yuko navyo kwa wakati fulani na vimewezaje kufika upande mwingine.
Kwa mfano, asilimia 10 ya watu waliokufa kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa SARS mwaka 2003, ukilinganisha na mafua makali ambayo yalikuwa chini ya asilimia 0.1.
Mazingira na mabadiliko ya tabia nchi yanabadilisha tabia ya wanyama ya namna wanavyoishi, maeneo wanayoishi na huwa wanakula nini.
Jinsi maisha ya binadamu yalivyobadilika pia, asilimia 55 ya idadi ya watu duniani kote wanaishi mjini na kuanzia asilimia 35 miaka 50 iliyopita.
Na miji mikubwa ina makazi mapya ya wanyama pori kama panya, fisi, nguchiro, ndege, nyani na wanyama wengine ambao wanaweza kuepo kwenye maeneo yanayozunguka jamii.
Wanyama hawa mara nyingi huweza kuwa karibu na mazingira ya binaadam kwa kuishi sehemu za kupumzikia na bustani na kuacha taka ambazo zinaweza kuwafikia binadamu.
Mara nyingi wanyama pori huwa wanaonekana katika miji zaidi ya porini kwa sababu kuna upatikanaji wa chakula kingi maeneo ya mjini na kufanya mzunguko wa upatikanaji wa magonjwa uwe rahisi.
Magonjwa mapya yanayojitokeza mara nyingi ni hatari zaidi ndio maana magonjwa mapya huwa yanapewa uangalizi wa karibu zaidi, huku baadhi ya makundi ya watu yakiwa kwenye hatari ya kupata magonjwa zaidi ya wengine.
Miji maskini inapaswa kufanyiwa kazi ya usafi kwa ujumla, kwa sababu kama mazingira si safi basi inakuwa rahisi kwa magonjwa yanyotokana na wanyama kuenea kwa kasi na kuathiri afya za wanadam.
Watu ambao wana mifumo dhaifu ya kutokuwa na afya nzuri wako kwenye hatari ya magonjwa zaidi, mfano mtu ambaye hana virutubisho vya mlo kamili, anaishi katika maeneo ambayo kuna hewa chafu na mazingira machafu.
Na wale watu ambao wakiugua huwa ni vigumu kupata huduma za kiafya nao wako kwenye hatari ya kuathirika kutokana maradhi kutoka kwa wanyama.
Maambukizi kutoka kwa wanyama kwenda kwa binaadamu yanaweza kusambaa katika miji mikubwa ambayo ina mkusanyiko mkubwa wa watu, ambao wanavuta hewa kwa pamoja na wako kwatika mazingira yanayofanana.
Baadhi ya tamaduni, watu huwa wanakula chakula ambacho wanahusiana na wanyama pori, ama pia wapo baadhi ya binadaam wanakula wanyamapori.
Jamii na serikali zinajaribu kukabiliana na maambukizi mapya ya magonjwa kuwa janga la kipekee linalohitaji kupewa uangalizi malum bila kuhusisha dalili zake kwa kuangalia mabadiliko yanayotokea katika ulimwengu.
Kadri mazingira yanavyobadilika, ndio magonjwa mapya pia yanaibuka. Kwa mfano asilimia 10 tu ndio ya magonjwa ndio imebainika kuwa ni mapya yanayohusishwa kutoka kwa wanyama.
Kuna umuhimu wa kuangalia jinsi magonjwa haya mapya yanaanzia wapi mpaka kufikia kuua watu katika maeneo ya mjini.
Kuweka mazingira kuwa safi ni jambo moja muhimu ambalo linaweza kusaidia kupunguza mripuko wa magonjwa na kusambaa kwake.
Lakini pia kubadili namna watu wanahusiana na wanyama katika mazingira yao ni jambo muhimu pia kuzingatiwa.