TASNIA ya muziki pamoja na kuwapatia umaarufu wanamuziki pia ni moja eneo lenye kuingiza kipato kikubwa wasanii kiasi cha wengine kuishi maisha ya kifahari sana.
Wanamuziki wote waliopata mafanikio hasa kwenda medani ya kimataifa wamekuwa na maisha mazuri na kuanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi.
Takwimu zinaonesha kwamba mnamo mwaka 2019, sekta hiyo ya muziki ilitengeneza zaidi ya dola bilioni 21 duniani kote, huku ikisemekana tasnia inakuwa kwa wastani asilimia 9 hali inayoongezea kipato zaidi.
Mwanamuziki kutoka nchini Uingereza Paul McCartney, hivi sasa ndiye anayechukuliwa kuwa mwanamuziki tajiri zaidi duniani akiwa na akiba ya utajiri kiasi cha dola bilioni 1.2.
Lakini jambo la kushangaza ni kwamba wanamuziki wengi hasa mashuhuri wamekuwa na mizozano ama wenyewe huita (bifu), wakati mwengine pasi na sababu za msingi.
Hatushangai kuwepo kwa bifu za wanamuziki kwa sababu sekta hiyo inawapatia kipato na wakati mwengine wanagawana mashabiki waliopo hivi mmoja wapo anaposhindwa kuzia bifu kwa lengo la kumuharibia mwenziwe.
Katika makala haya nataka nikuletee baadhi ya bifu za wanamuziki na kusababisha wanamuziki hao kuwa na ugomvi wa muda mrefu.
Mnamo mwaka 2017 wanamuziki wa kike kutoka nchini Marekani Cardi B na Nicki Minaj waligombana hadhani wakitumiana maneno kiasi cha kutaka kuingiliana mwilini.
Ugomvi wao ulidhihirika kwenye tamasha la kwenye tamasha la wiki ya fesheni nchini Marekani lililofanyika mjini New York katika mwaka 2017, ambapo wanamuziki hao inasemekana walipigana baada ya kuona hakutoshi kushambuliana kwa maneno.
Video iliochapishwa katika jarida la TMZ nchini Marekani ilionyesha wawili hao wakirushiana cheche za maneno huku Cardi B baadaye akilazimika kumrushia kiatu chenye kisigino Minaj baada ya kupigwa kisugidi cha uso na mlinzi wa kuweka usalama.
Hata hivyo kwenye ugomvi huo Minaj alionekana kana kwamba hana habari, ambapo wawili hao waliendeleza vita vyao katika mitandao ya kijamii hususan instagram ambapo walirushiana cheche kali za maneno.
Mgogoro mwengine mkubwa uliowahusu wanamuziki ni baina ya Lady Gaga na mwanamziki mkongwe Lady Madonna.
Wakati Lady Gaga alipotoa kibao cha ‘Born This Way’ mwaka 2011, watu wachache walifikiria kwamba ni wimbo unaojulikana, mmoja wao akiwa Madonna, ambaye aliona kwamba wimbo huo unafanana na ule wake wa 1989 kwa jina ‘Express Yourself’ ambapo alioucheza aliweka nyimbo hizo pamoja katika ziara moja.
”Wakati ambao nilimkosoa Lady Gaga ni ule ambapo nilihisi kwamba ameimba wimbo kama wangu”, Madonna alisema 2015. ”Sio kana kwamba anachukua nafasi yangu ama anachukua taji langi. Anaimba nyimbo zangu, sidhani kwamba ana kipaji kikubwa cha uimbaji ama mtunzi.
Madai hayo ya Madonna ndiyo yaliyosababisha Lady Gaga naye kuja juu ambapo kwa miaka kadhaa wanamuziki hao wakaingia kwenye bifu.
Gaga ambaye kwa jina lake ni Stefani Germanotta- katika makala yake ya Five Foot Two, yaliotolewa alisema kuwa hakufurahia kwamba Madonna hakuzungumza naye moja kwa moja.
”Licha ya heshima ninayompa sikudhania kwamba anaweza kusema kitu bila kukutana nami na kuniambia makosa yangu”, alisema.
Bifu jengine ni baika ya mwanadada Taylor Swift na rapa wa kiume Kanye West ambao lilianza mnamo mwaka 2009, kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za MTV.
Kanye hakufurahishwa na ushindi wa Taylor wa kanda ya video ya mwaka kwa jina ‘for You Belong with Me’. Alidhani badala yake ni Beyonce aliyefaa kuibuka mshindi kupitia kanda yake kwa jina ‘Single Ladies’.
Na kama tunavyojua, Kanye sio mtu anayeficha hisia zake. Rapa huyo alipanda jukwani wakati wa hotuba ya Taylor ya kukubali ushindi huo, akachukua kipaza sauti na kiusema: Taylor nafurahi sana na nitakuwacha umalize, lakini Beyonce alikuwa na kanda nzuri sana ya video katika historia.
Wawili hao baadaye walikutana na kupatana, lakini miaka michache baadaye West alidai katika kibao chake kwamba hatua aliyochukua ilimsaidia sana Taylor Shift katika kazi yake.
Taylor alidai kwamba hakuyapatia baraka maneno ya wimbo wa West kabla utoke, lakini mkewe rapa huyo Kim Kardashian alichapisha ujumbe katika snapchat ambao ulioonekana ukimuonyesha Taylor akiubariki wimbo huo.
”Katika tuzo za Grammy, Swift alijibu: Nataka kuwaambia wasichana wote -kutakuwa na watu katika kazi yenu ambao watajaribu kukuvurugia ufanisi wenu ama hata kujisifu kwa manufaa yako ama hata umaarufu, endeleeni kufanya kazi zenu bila mtu kuwaingilia kati ili kuwavunja motisha”.
Taylor baadaye alimkejeli Kanye katika wimbo wake ‘Look What You made me do’. ”Sipendelei jukwaa lako lililojuu chini, na jukumu ulilochukua”, aliimba.
Mzozo mzwengine ni ule wa wanamuziki Zayn na Naughty Boy ambapo mwaka 2015, Zayn Malik alianza kufanya kazi na Naughty Boy ambaye ni mtayarishaji maarufu wa muziki.
Lakini ni vyema kusema kuwa yeye na Zayn hawakufanikiwa kufanya mazuki pamoja.
“Naughty Boy una mzaha sana wacha kujidai kwamba wewe ni rafiki yangu hakuna mtu anayekujua, Zayn alichapisha ujumbe wa Twitter baada ya kukosana wakati wa kurekodi.
Boy baadaye aliambia gazet la The Guardian kwamba kijana huyo mwenye umri anatupatupa maneno na kwamba walikuwa wamekosana kutokana na ushawishi kutoka nje.
Mgogoro mwenfine ni Azealia Banks na Iggy Azalea, ambapo idadi ya nyota ambao Azealia Banks amekosana nao ni kubwa mno hali ya kwamba inaweza kuandika orodha. Lakini mtu ambaye alikosolewa sana na mwimbaji huyo ni msanii Iggy Azalea.

Kwa wasanii wawili ambao walikuwa maarufu wakati mmoja na walikaribia kuwa na jina moja, walikuwa na tofauti kubwa na hawakuweza kulinganishwa kivyovyote.
Bifu yao ilianza wakati jarida la XXL lilipomuweka Iggy katika ukurasa wake wa kwanza wa jarida lao la kila mwaka ambalo linawaangazia wasanii wapya katika muziki kila mwaka.
Banks hakupendelea sana uamuzi uliochukuliwa na mhariri wa jarida hilo. Alisema kuwa jarida hilo lilikuwa limekosea kumweka Iggy na kuendelea kumshutumu kwa kukiuka tamaduni ya weusi.
Iggy Azelea alijibu kwa kusema: “Huwezi kuzuia baraka zangu, nasherehekea, elewa ama jipange”. Mgogoro wao uliendelea kwa miaka kadhaa , huku Iggy akidai kwamba mwaka 2014 ufanisi wake mkubwa 2014 ndio sababu ya Banks kutaka kujipatia umaarufu.
Bifu jengine ni Benzino na Eminem. Hakukukosa mgogoro wa Rap mapema miaka ya 2000. Nas na Jay Z. DMX na Ja Rule. 50 Cent dhidi ya marapa wengine wote.
Lakini mgogoro mkubwa kabisa ulihusisha majina makubwa katika sanaa ya muziki wakati huo na mwanamuziki mwingine ambaye hakuwa maarufu kwa jina Benzino – Mwanzilishi mwenza wa gazeti la mtindo wa hiphop la The Source.
Benzino aliachilia muziki uliomdhalilisha Eminem kwa jina Pull Your Skirt Up, ambao ulimtaja Eminem kuwa Vanilla Ice ya 2003 na kumlinganisha na mwanamke.
Eminem alijibu kupitia kibao chake Nail in the Coffin, ambapo alisema hakuna mtu anayetaka kumsikiliza babu yake akirap.
Bifu jengine ni baina ya Lil’ Kim na Nicki Minaj. Iwapo Rappa yeyote mpya ambaye ni mwanamke atawasili katika sanaa ya muziki huo na Lil Kim hajaanza vita naye-basi hajawahi kuonekana.
Kim ana historia ya kugombana na Eve, Foxy Brown, Remy Ma na wengine wengi. Lakini hao walikuwa watu wadogo ikilinganishwa na Nicki Minaj kama ilivyoonekana.
Albamu ya Nicki kwa jina ‘Pink Friday’ ilipata ufanisi mkubwa wakati ilipotolewa 2010, lakini Lil Kim hakufurahia.
Katika wimbo aliouweka katika mitandao ya kijamii kwa jina ‘Black Friday’, Kim alimtaja Nicki kuwa mtu ambaye anataka kuwa kama Lil Kim kwa kuwa anamuigiza ambapo Minaj, alijibu kwa kumuita ‘kahaba mjinga’.

Bifu jengine ni baina ya warembo wawili Rihanna na Ciara. Cha kumalizia ni kwamba RiRi na CiCi, wote walianza muziki mwaka 2005 huku Ciara akipanda katika chati za muziki na wimbo wake ‘Goodies’, Rihana naye akiwa katika nafasi ya pili na wimbo wake ‘Pon De Replay’.
Walikuwa wasichana wadogo waliokuwa na matumaini makubwa ya muziki wa R&B na pia walikuwa wakienda kujivinjari pamoja,lakini miaka michache baadaye mambo yalibadilika na kuwa mabaya
“Nilikutana naye na hakuwa mzuri,”Ciara alisema 2011. “haukuwa mgongano mzuri.” Baadaye walianza kujibizana katika mtandao wa Twitter. Rihanna: “Ciana, je nilisahau kukupa ushauri.?”
Ciara: “Kweli Rihanna usingependelea kukutana nami mahala popote ama katika jukwaa..”
Rihanna: ” We gangsta huh?… kila la kheri katika jukwaa unalozungumzia.”
Lakini haikuchukua muda kabla ya Rihanna kurudi nyuma na kuandika: “Ciara baby, nakupenda! Ulinikosea sana katika runinga. Pole sana!”
Ciara alijibu: ‘Rhi, unajua tumekuwa tukipendana tangu siku ya kwanza! Ulinikosea sana katika sherehe ile! msamaha wako umekubaliwa. Tuzungumze ana kwa ana.”Huoni kama huo ni upendo tuwe marafiki