LONDON,UINGEREZA

KULINGANA  na takwimu jumuishi za hivi karibuni za shirika la habari la Reuters, jumla ya watu milioni 26.75 wameambukizwa virusi vya corona ulimwenguni kote.

Waliofariki duniani kote kutokana na ugonjwa wa COVID-19 ni watu 875,419.Mexico ilithibitisha maambukizi mapya 6,319 na vifo vipya 475.

Idadi ya vifo iliongezeka nchini humo na kufikia 67,326. Nchini India maambukizi yalipindukia milioni nne, hali ambayo inaongeza changamoto kwa taifa hilo.

Mfumo wa afya wa India hauna ufadhili wa kutosha na hivyo unazidi kuelemewa.

Awali, virusi vya corona viliathiri zaidi miji yenye idadi kubwa ya watu, lakini sasa virusi hivyo vilisambaa katika karibu kila jimbo hadi miji midogomidogo na vijijini.

India sasa ni nchi ya tatu ambayo idadi ya maambukizi imepindukia milioni nne baada ya Marekani na Brazil.