RAMALLAH,PALESTINA
MAELFU ya wakaazi wa Palestina wamefanya maandamano makubwa na kukusanyika mbele ya makao ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kutoa wito wa kujizulu kiongozi huyo.
Waandamanaji hao wenye hasira huku wakiwa wamebeba mabango walisikika wakipiga kelele dhidi ya Benjamin Netanyahu na kumtaka ajiuzulu wadhifa wake huo na kujitenga kabisa na siasa kutokana kukabiliwa na tuhuma za ufisadi.
Katika miezi ya hivi karibuni Israel imekuwa ikishuhudia maandamano makubwa ambayo yanamtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ajiuzulu kutokana na waandamanaji kushindwa kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Maandamano hayo yanafanyika kila Jumapili na kuhudhuriwa na maelfu ya watu. Netanyahu na baraza lake la mawaziri wanalaumiwa kwamba, badala ya kutanguliza mbele matatizo ya kiafya na kiuchumi yanayoisumbua Israel kwa sasa, wameng’ang’ania kusukuma mbele gurudumu la mipango ya kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Taarifa zinaeleza kuwa, chama cha Bluu na Nyeupe cha Benny Gantz ambacho kinahesabiwa kuwa muitifaki wa Netanyahu katika kuunda serikali na ambaye ni Waziri wa Vita kimetangaza kuunga mkono maandamano hayo yaliyo dhidi ya Netanyahu, msimamo ambao unaonesha ni kwa jinsi gani Serikali ya Waziri Mkuu wa Israel inakabiliwa na mgawanyiko.