NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya Machicha imefanikiwa kutinga hatua ya Robo fainali ya Mashindano ya Coco Sport Ndondo Cup, baada ya kutoka na ushindi wa mikwaju ya penalti 4-3 dhidi ya Sky Way Mauzo.

Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Kiembe Samaki majira ya saa 10:00 jioni ambao uliokuwa wa ushindani kwa timu hizo.

Hadi timu zinakwenda mapumziko hakuna aliyefanikiwa kuzifumua nyavu za mwenzake.

 Kurudi uwanjani kumalizia kipindi cha pili timu hizo zilingia na mabadiliko,huku kila mmoja akiamini atafanya vyema na kushinda mchezo huo,lakini dakika 90 zilimalizika hakuna aliona bao la mwenzake.

Kwa matokeo hayo muamuzi wa mchezo huo alitumia sheria ya mikwaju ya penalti na Machicha kupata ushindi huo na kuendelea na mashindano.

Mchezo mwengine uliopigwa kati ya Katalunya na Taifa Tangini,timu ya Katalunya ilifanikiwa kuendelea na hatua ya robo baada ya kutoka na ushindi wa penalti 5-4.