TRIPOLI,LIBYA

RAIS Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema anataka kwa pamoja na majirani wa taifa la Libya kushiriki katika kutafuta suluhisho la mgogoro wa taifa hilo.

Katika hotuba yake aliyoitoa hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa alisema ni matarajio yake kwamba jitihada hiyo iongozwe na Ufaransa kwa ushirikiano wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika wiki kadhaa zijazo.

Na kuongeza pia kwa kuyaleta pamoja mataifa yote jirani, kutasaidia kwa kiwango kikubwa katika upatikanaji wa amani ya Libya.

Hata hivyo katika hotuba yake hiyo Macron hajasema ni nchi gani hasa anazotaka zihusike katika mazungumzo hayo na wala hajatoa ufafanuzi zaidi wa mpango huo.