NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba Queens, Mussa Mgosi amefunguka kuwa wachezaji wa kike wenye hulka za kiume hawana nafasi kwenye kikosi chake.

Wachezaji wengi wa soka la wanawake wamekuwa wakivaa mavazi ya kiume na kujiweka kwenye muonekanao huo ambao unawakwaza watu wengi.

Akizungumza na Zanzibar Leo Mgosi, alisema Simba ni timu kubwa hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa mfano wa kuigwa na sio kuwa wavunja nidhamu.

Alisema moja ya masharti ya kucheza kwenye kikosi chake ni kuwa na nidhamu ya kutosha kwa kuwa kwenye muonekano wa kike.

Alisema nidhamu ndiyo ambayo imefanya kuwa na timu bora katika soka la wanawake tangu alipo jiunga na kikosi chake hicho.

“ Simba ni timu kubwa na inahitajika kuwa mfano wa kuigwa moja ya mambo ambayo ninayazingatia ni nidhamu, mchezaji anae jiweka kiume kwenye timu yangu hana nafasi labda akubali kubadilika,” alisema

Simba Queens ndio mabinga wa Soka la Wanawake Tanzania Bara kwa msimu uliopita.