YERUSALEMU,ISRAEL
MAHAKAMA moja katika utawala wa Israel imetoa amri ya kubomolewa msikiti mmoja ulioko mashariki wa Quds Tukufu inayokaliwa kwa mabavu.
Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini katika Ukanda wa Gaza ililaani vikali uamuzi huo wa mahakama, wa kutoa agizo la kubolomewa Nyumba Tukufu ya waumini wa Kiislamu katika mji mtukufu wa Quds unaokaliwa kwa mabavu na utawala huo.
Mahama hiyo ya Israel inadai kuwa, msikiti huo Qaqaa Bin Amr ulioko mjini Silwan ulijengwa bila kibali cha ujenzi kutoka kwa utawala huo.
Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini katika Ukanda wa Gaza iliitaka jamii ya kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) kuyalinda maabadi na maeneo matakatifu ya Kiislamu mjini Quds.
Utawala pandikizi wa Israel uliwapa wakaazi wa mji huo siku 21 kukata rufaa ya kupinga uamuzi huo, vinginevyo agizo hilo la kubomolewa msikiti utekelezwe.
Msikiti huo ambao ulijengwa mwaka 2012, una uwezo wa kubeba mamia ya waumini wa Kiislamu kwa wakati mmoja.