RIYAD, SAUDI ARABIA
SAUDI ARABIA imetangaza mipango ya kurejesha taratibu ibada za hija za Kiislamu kwenye mji mtakatifu wa Makka kuanzia mwezi ujao.
Serikali ya Saudi Arabia ilisitisha ibada hizo mwezi Machi kutokana na mripuko wa virusi vya corona.
Iliwapiga marufuku wageni wote wa kimataifa kuingia nchini humo kuhiji ili kupunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya mahujaji.
Licha ya hayo lakini Serikali ilitangaza mipango ya kuwaruhusu waumini nchini humo kuhudhuria ibada hizo kuanzia mwezi ujao.
Idadi ya ukomo wa watu 6,000 kwa siku utawekwa kuwezesha watu kuwa mbali mbali.
Kuanzia Novemba mwaka huu Saudi Arabia itaruhusu wageni kutoka nchi kadhaa kwenda kufanya hija kwa ukomo wa watu 20,000 kwa siku.