“NAAMINI Celine ataweza kufanya kazi vizuri bila kuwa na mimi”, alisema Rene Angelil katika shoo 40 alizotumbuiza mwanamama huyo, kuanzia Agosti 27 hadi Januari 2016 wakati mume wake akipigania maisha yake.


Utabiri huo kwa bingwa wa miondoko ya R&B Marie Claudette Dion umekuwa kweli pale alipoachia albam mpya “Courage” ya kwanza tangu meneja wake na mumewe alipopoteza vita yake na saratani Januari 14, 2016 njia ndefu ya meneja huyo kumfikisha kileleni Celine Dion ikafika mwisho.


“Kiukweli naogopa sana kumpoteza mume wangu!” Ingawa nimemhakikishia kusimama imara pindi atakapoondoka kilinukuliwa chanzo kilichokuwa karibu na Celine wakati mumewe akipigania uhai wake. Alitaka niendelea kuimba baada ya yeye kuondoka,
“Ni kama, wakati siko jukwaani, mashabiki wangu wako nyumbani ninaenda hotelini kwa mfano, sina mazungumzo na mtu.” Mrembo huyo alifichua kuwa anakosa kila kitu kutoka kwa mumewe na meneja wake huyo.


Alipohojiwa na Gayle King katika kipindi cha “This morning” kinachorushwa na televisheni ya CBS kuhusu albamu yake mpya na ya kwanza bila Renne, alianza kwa kuzungumzia maisha yake na Renne.


Alisema harufu yake, mguso wake vilimsababisha acheke, mrembo huyo alifunua yaliyo moyoni mwake kutokana na kuwa na maisha ya kutokuwa na mpenzi wake aliyetengana naye kwa sababu ya kifo.


Albam hiyo iliyopambwa na wimbo “Courage” ina vibao vyengine vikali kama vile “Flying on My Own”, “Lovers Never Die”, “The Chase” na nyingine zinazodhihilisha umahiri wa sauti ya mwanamama huyo anayeelekea uzeeni.


Licha ya uchungu alio nao, Dion alisema yuko tayari kupata mapenzi mwengine mpya”. “Rene atakuwa nami kila siku, lakini sina uchungu, akimaanisha kutomuona kimwili.
Akizungumza kwa kujiamini anavyofanya kazi bila meneja wake yaani Renne na jinsi anavyojielekeza alisema anajiambia hivi: Acha maumivu, Sema ndio. Sema ndio kwa kucheza. Sema ndio kwa urafiki,”, “Sema ndio kwa upendo labda siku moja. Sijui.”


“Je! Uko wazi kwa hilo?” King aliuliza kwa mshangao bila kuamini kama kweli maneno hayo yanatamkwa na na Celine anayemfahamu!.
“Ndio,”. “Nafungua kitabu … niko wazi. Niko tayari? Hapana? Itatokea? Sijui. Lakini sina msisitizo hata kidogo. Ninafurahia maisha yangu ya sasa zaidi kuliko awali”, anajibu.


Awali ET ilipozungumza na Dion mnamo mwezi Septemba mwaka alisisitiza taarifa hizo, na kubainisha kuwa ingawa “hatapata mapenzi kama ya Rene tena hapa duniani lakini anafuraha maishani mwake.


“Nimo katika mapenzi, ninapenda maisha yangu, ninapenda watoto wangu, ninapenda kazi yangu. Ninapenda kile ninachofanya leo hata zaidi kuliko awali.


“Je! Nitakuwa na mwenza mwengine katika maisha yangu? Tuache ilivyo, nikifanya hivyo itakuwa raha kushiriki hilo”,alisema. “Ni sura ambayo imefungwa, lakini sio kitu ambacho kimekufa. Unabadilika na labda wakati mwingine unakutana na rafiki na inabadilika kuwa kitu kikubwa kuliko hicho. Nani anajua labda sivyo? Lakini nitakujulisha. Ninaahidi.”


Mahojiano na CBS yalifanyika siku chache kabla ya mwanamziki huyo huyo kuachia albam yake mpya ya “Courage” inayoambatana na safari ya kwanza ya maonyesho kadhaa tangu kifo cha mumewe na meneja wake Rene Angelil.


Dion anasema “Ilinibidi nijithibitishie mwenyewe kuwa naweza. Nilihitaji kudhibitishia familia yangu, marafiki, wafanyibiashara, tasnia ya muziki, mashabiki … kwamba naweza kuimba na kuendelea na sio kugangaganga tu, lakini ni kazi, “alisema. “Ninahisi kama naweza kufanya chochote ninachotaka. Niko vizuri kila wakati na nitakuwa vizuri wakati wote.”


“Ninapoangalia nyuma, familia yangu imepitia mengi, kumpoteza mume wangu, meneja wangu, baba wa watoto wangu na rafiki yangu,” “Ninahisi mtetemo wake na msaada wake,”alisema.
‘Courage’ ni albamu ya kumi na mbili kwa lugha ya kiingereza ya Celine Dion, iliyofyatuliwa na studio ya Columbia Novemba 15, 2019.