NA JOSEPH NGILISHO,ARUSHA
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amezindua kampeni za ubunge katika jimbo la Arusha mjini, na kueleza serikali ilivyotekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa maji wa shilingi bilioni 525.
Alisema azma ya serikali kuwaletea maendeleo katika nyanja za elimu ,vituo vya Afya na Miundo Mbinu na Barabara.


Majaliwa ameyasema hayo wakati akizindua kampeni za ubunge na kumnadi mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini Mrisho Gambo katika viwanja vya Relini ndani ya jiji la Arusha Jana.
Alisema kuwa “nipo mbele yenu kumuombea kura rais wetu Dk.John Magufuli siku ya tarehe 28 mwezi Oktoba, sina shaka na ombi langu hilo kwenu kwa sababu mnapenda maendeleo”.


Majaliwa ambaye pia ni Mjumbe wa mkutano Mkuu wa Taifa CCM alisema mmeona kazi alizofanya ndani ya kipindi cha miaka mitano kwa kutekeleza ilani ya chama chetu kwa kishindo kipindi cha 2015/20


Alisema Dk.. Magufuli anao uwezo wa kusimamia maendeleo na uwezo wa kugusa nyozo za Watanzania na matamanio ya rais wetu ni kusogeza huduma za Afya
Aidha serikali imejenga zahanati 1950 vituo vya Afya 498 vikiwa na majengo yote muhimu vyumba vya maabara upasuaji na mama na mtoto tumejipanga vizuri


Naye aliyekuwa mtia nia wa ngazi ya ubunge jimbo hilo na mgombea ubunge wa jimbo hilo mwaka 2015 ,Philemon Mollel Monabani, alisema kuna vitu vitatu anaviogopa sana hapa duniani ,ikiwa ni pamoja na wajumbe walioshiriki kuwachagua wagombea.


Hata hivyo alisema hana kinyongo tena na uchaguzi wa kura za maoni ambao umeshapita na kwa sasa wameungana na kuwa kitu kimoja na kuwataka wananchi kumchagua Rais John Magufuli ambaye alimbatiza kuwa ni nabii sababu maendeleo aliyoyafanya yameonekana.


Naye Meya wazamani wa Arusha,Gaudence Lyimo ambaye pia alikuwa mtia nia wa ubunge hilo, alisema wataendelea kumuombea kura Rais wetu Dk. John Magufuli, waubunge pamoja na madiwani ili kuifanya Arusha iendelee kuwa ya kijani.


Aliyekuwa meya wa Arusha Kalist Lazaro Meya Mstaafu alisema watamsaidia Mrisho Gambo kupata kura za kishindo pamoja na Madiwani wa chama cha mapinduzi Dk.Magufuli
Naye Abdulrahman Kinana aliwataka wana Arusha kuchagua watu watakaoleta maendeleo, kwa kupima yale yaliofanywa kwa miaka mitano.