NA KHAMISUU ABDALLAH

FAINI ya shilingi 400,000 imemshukia Bakar Ali Makame (24) mkaazi wa Sebleni baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matano ya usalama barabarani.

Mshitakiwa huyo alifikishwa katika mahakama ya wilaya Mwanakwerekwe mbele ya Hakimu mdhamini wa mahakama hiyo Mohammed Subeit na kusomewa mashitaka yake na Mwendesha Mashitaka Wakili wa Serikali Soud Said.

Alidai kuwa, Septemba 16 mwaka huu, saa 4:30 asubuhi huko Mazizini Polisi akiwa dereva wa gari yenye namba za usajili Z 420 HC P/V akitokea Kiembesamaki kuelekea Migombani alipatikana akiwa andesha gari hiyo barabarani ikiwa hana leseni ya udereva kitendo ambacho ni kosa kisheria.