Ampigia debe Dk. Hussen, awaomba wananchi kumchagua kwa kishindo

Na Rajab Mkasaba

“MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ni mtu makini, mwenye uzoefu katika uongozi na anapenda maendeleo na Dk. Magufuli nae tunamuelewa vyema uwezo mkubwa alionao wa kuwaletea maendeleo Watanzania”.

“Siku ikifika twendeni tukawapigie kura kwa wingi pamoja na wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani kwa tiketi ya CCM”.

“Tuwachagueni ili kuendeleza mafanikio tuliyoyapata na kuendelea kudumisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania kwa dhamira ile uile ya Waasisi wetu.CCM pekee yake ndio inayoweza kuzidumisha tunu hizi muhimu.

Hayo ni maneno ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein aliyoyatoa katika hotuba yake kwa nyakati tofauti katika Kongamano la wanawake lililofanyika katika Ukumbi wa Makonyo Wawi Pemba na lile lilolofanyika katika Ukumbi wa CCM, Amani Mkoa mjini Unguja.

Katika hotuba zake hizo Mama Shein mbali ya kueleza maudhui ya Kongamano hilo pia, alitumia fursa hiyo kuwataka akina mama kuhakikisha wanaendelea kukipa ushindi chama chao cha CCM kwa kuwapigia kura viongozi wake wote wanaogombea nafasi tofauti.

Mama Shein amekuwa akisisitiza kwamba ni vyema wagombea wote hao wakapewa ushirikiano unaohitajika ili CCM iendelee kuongoza Dola hasa ikifahamika kwamba chama hicho ndio chama pekee chenye malengo ya kuendeleza Muungano, Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964 sambamba na maendeleo yote kwa jumla.

Kwa maelezo ya Mama Shein Umoja na mshikamano ni mambo ya msingi katika kukipatia ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia, Wagombea wa nafasi mbali mbali ni vyema wayavunje makundi yao na wawaunge mkono wagombea wote waliopitishwa na CCM.

“Kama tunavyoelewa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Mheshimiwa Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ni mtu makini, mwenye uzoefu katika uongozi na anapenda maendeleo kila mmoja wetu anajua jukumu alke wakati ukifika”alisema Mama Shein.

“Kwa lengo la kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi unaokuja, kwanza lazima tuendelee kuwa wamoja. Kwa mnasaba huo, naunga mkono kauli mbiu ya mkutano isemayo ”Umoja wetu wanawake ndio ngao yetu”, alisisitiza Mama Shein.

Aidha, Mama Shein aliendelea kueleza kuwa kauli mbiu hiyo ni muhimu kutokana na ukweli kwamba wanawake wakiwa wamoja kutokana na wingi wao watakiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kishinde vizuri katika nafasi zote za uongozi katika uchaguzi Mkuu unaokuja mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020.

Hivyo, aliwasisitiza wanawake kutambua kuwa ni wajibu wao wote kutilia mkazo kauli mbiu hiyo kwa kuepukana na ubinafsi, makundi na waweke mbele maslahi ya CCM wakizingatia maneo ya wazee yasemayo “Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”.

Aliwataka wanawake kwua wamoja ili wapate nguvu za kukabiliana na siasa za kubaguana, kasumba na uongo ambao husemwa na baadhi ya wasiopenda maendeleo dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliwafahamisha wanawake hao wa CCM pamoja na wananchi wote wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jumla kwamba wote ni mashahidi juu ya mafanikio ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba.

Mama Shein anaeleza kuwa CCM imetekeleza Ilani, ahadi na sera zake kwa usawa kiasi kwamba kilichofanywa Unguja na Pemba vile vile kimetekelezwa.

Anaongeza kuwa iwe maji safi na salama, huduma za afya, elimu, miundombinu, kilimo, uwezeshaji na sekta nyengine zote na kusisitiza kwamba Serikali za CCM hazina ubaguzi na badala yake huleta maendeleo kwa watu wote. “Kwa hivyo, tuungane tuipe CCM ushindi ili ituletee maendeleo zaidi”, anaeleza Mama Shein.

Sambamba na hayo, Mama Shein aliweza kusisitiza umuhimu wa kuwa na umoja na mshikamano katika kukipatia ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na kuwaunga mkono wagombea wote waliowekwa kwa tiketi ya CCM katika ngazi zote za uongozi, ili wapate ushindi mkubwa.

Anasisitiza kwamba viongozi wote ni watu makini na wameonesha uwezo na umakini na umahiri mkubwa katika uongozi.

Mama Shein anawataka wanawake wote wa CCM pamoja na wananchi wengine kuwapa ushirikiano unaohitajika wagombea wote  wa nafasi mbali mbali waliopitishwa na CCM kwani chama hicho ndio chama pekee cheye malengo ya kuuendeleza Muungano wa Serikali mbili, Mapinduzi matukufu ya tarehe 12, Januari 1964 na maendeleo kwa jumla.

Mama Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa akina mama hao kwa kuchagua kauli mbiu nzuri ya Kongamano hilo isemayo “Umoja wetu Wanawake ndio nguvu yetu”,alisema Mama Shein.

Aidha, Mama Shein alikubaliana na kauli mbiu hiyo kutokana na ukweli na umuhimu wake kwa ukweli kwamba wanawake wakiwa pamoja, ndop watakuwa na nguvu Zaidi ya kufanya uwamuzi unaofaa, kwa faida ya wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa maelezo ya Mama Shein uwamuzi unaofaa kwa hivi sasa ni kukipa Chama Cha Mapinduzi ili kishinde vizuri, katika nafasi zote za uongozi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu wa 2020.

“Tusiasahau maneno ya Wazee wetu yasemayo ”Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”, alisisitiza Mama Shein.

Mama Shein anasisitiza kwamba umoja na mshikamano ni mambo ya msingi katika kukipatia ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM), anaeleza kuwa wagombea wa nafasi mbali mbali ndani ya chama hicho ni vyema

Jambo jengine ambalo Mama Shein alisisitiza ni umhimu wa kuitunza Amani iliyopo hivi sasa, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.

Mama Shein anaeleza kuwa bila ya Amani, hakuna jambo lolote linaloweza kufanikiwa kwani wanawake na watoto mara nyingi ndio wanaopata shida Zaidi pale Amani inapoondoka.

Kwa hivyo, Mama Shein anaeleza kwamba ni wajibu wao kujiepusha wao na watoto wao pamoja na familia zao na mambo yanayoweza kusababisha kuvunjika kwa Amani.

“Tumuombe Mwenyezi Mungu atujaalie tuweze kushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa Amani na utulivu na kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kushiriki na kuendelea kushika Dola”.

Mama Shein aliweza kutumia fursa hiyo kumpongeza Mke wa Mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Mama Maryam Hussein Mwinyi kwa uwamuzi wake wa kujumuika na akina mama hao katika Kongamano lililofanyika kisiwani Pemba.

Katika maelezo yake Mama Shein alimueleza Mama Maryam Mwinyi kwa niaba ya wanawake wote wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), pamoja na wake wa viongozi wa chama hicho cha CCM, wanamkaribisha.

Pia, wanwake hao wanamuhakikishia kwamba wamefurahi kuwa pamoja nae na watafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar pamoja na wagombea wote wa chama hicho wanapata ushindi wa kishindo ili kuiwezesha CCMmba kuendelea kushika Dola.

MKE wa Rais Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akihutubia
katika hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania 
(UWT)  “Umoja Wetu Wanawake Ndio Nguvu Yetu”lililofanyika katika ukumbi
wa Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Jijini Zanzibar. Lililowashirikisha
Viongozi wa UWT na Wagombea Ubunge na Uwakilishi Zanzibar. (Picha na
Ikulu).

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania Mhe. Gaudentia
Kabaka akimtambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Mhe.Hussein Ali Hassan Mwinyi na (kulia kwa Mgombea)
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Mke wa Makamu wa Pili wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, wakati wa hafla ya Kongamano la
“Umoja Wetu Wanawake Ndio Nguvu Yetu”) lililofanyika katika ukumbi wa
Afisi ya CCM Mkoa wa Mjini Amani Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)