LONDON, England
MANCHESTER City wamemsaini mlinzi wa umri wa miaka 23, Ruben Dias kutoka Benfica kwa mkataba wa miaka sita wa pauni milioni 65.

Mlinzi wa kati wa Argentina, Nicolas Otamendi amehamia njia nyingine kwa pauni milioni 13.7.
Dias anakuwa usajili wa tatu muhimu wa majira ya kiangazi wa bosi wa ManCity, Pep Guardiola, kufuatia kuwasili kwa beki, Nathan Ake na mshambuliaji, Ferran Torres.

“Kupata nafasi ya kujiunga na klabu kama Manchester City ni fursa nzuri kwangu na ambayo sikuweza kukataa”, alisema, Dias. “Mafanikio yao yanajisemea yenyewe. Wamekuwa timu kubwa nchini England katika miaka michache iliyopita, wakicheza chapa ya kushambulia ambayo ninahisi inafaa kwenye mchezo wangu mwenyewe.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alihitimu kutoka akademia ya Benfica kabla ya kucheza mechi 113 za wakubwa, na kushinda taji la Ureno mnamo 2018-19.

Ameshinda pia mechi 19 akiwa na Ureno na ataimarisha ulinzi wa ManCity ambayo iliruhusu magoli matano katika kipigo chao cha hivi karibuni dhidi ya Leicester City.(BBC Sports).