ZAIDI ya mwezi mmoja sasa baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi katika taifa la Mali liliopo magharibi mwa bara la Afrika, lakini kabla ya mapinduzi hayo nchi hiyo ilikuwa kwenye mapambano dhidi ya makundi yenye itikadi kali.
Baada ya mapinduzi hayo, viongozi wa jeshi nchini humo wanasisitiza kuwa mapambano dhidi ya makundi yenye itikadi kali yanaendelea, lakini suala la kurejesha demokrasia bado linaonekana kuwa tete.
Hatua ya mwisho itakayotoa mustakabali wa Mali kupitia uongozi wa mpito kuelekea uchaguzi mkuu mpya baada ya wanajeshi kuchukua madaraka mjini Bamako, na kumlazimisha Rais Ibrahim Boubacar Keïta kujiuzulu haijafikiwa.
Wanajeshi hao wanaamini wataushawishi muungano wa jumuiya ya kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kukubali mpango wao, baada ya mazungumzo.
Lakini kutoka nje, hatua hiyo imatuma ujumbe wa wazi kwa washirika wa kimataifa ambao wana maelfu ya wanajeshi waliopelekwa maeneo ya kaskazini mwa Mali kukabiliana na mzozo wa kiusalama wakati wakishambuliwa na makundi ya kijihadi wakati maeneo ya kati yanahofia kuzuka kwa mapigano ya kikabila na vurugu
Meja kanali Ismaël Wagué, msemaji wa jeshi la kitaifa lilojitangazia kukomboa wanachi (CNSP), alisisitiza kuwa vikosi vya kulinda usalama vya Umoja wa Mataifa nchini Mali, vikosi vya kupambana na vikosi vipya maalum vya Ulaya vinavyoendesha oparesheni katika eneo hilo vilikuwa ‘vinashirikiana kuleta uthabiti.
Zaidi ya mwaka mmoja sasa kumekuwa na ishara kwamba raia wa Mali wanachukizwa na uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika nchi yao, licha ya jukumu wanalotekeleza kama mshirika muhimu na wakati mwingine kuonekana kuchua jukumu la vikosi vya taifa.
Lakini Kanali Wagué anajiepusha na hoja hizo ambazo zinazoibua na kuongeza zaidi katika taifa hilo linalozongwa na changamoto kadhaa kwa wakati huu.
Aliweka wazi kwamba viongozi wapya wa kijeshi wako tayari kuedelea kufanya kazi kwa karibu na vikosi vya kimataifa sawa na vile wanavyotarajia kuafikiana na ECOWAS katika mpango wao utakaotoa muelekeo wa kisiasa wa siku zijazo.
Japo makubaliano ya mwisho na muungano wa kikanda juu ya masharti ya mpito yanaonekana kulega lega bado tishio kutoka kwa makundi ya kijihadi linaendelea kuwapo.
Kwa hivyo harakati za kijeshi katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo zinaendelea na inasadikiwa kuwa bado ni oparesheni hatari.
Wanajeshi wawili zaidi wa Ufaransa waliuawa kutokana na bomu la kutegwa pembeni ya barabara katibu na mji wa Taoudenni Septemba 5 mwaka huu, ikiwa ni tukio la hivi karibuni.
Katika mzozo huo ambao umesababisha vifo vya wanajeshi 45 wa Ufaransa na kuwajeruhi wengine wengi kutoka vikosi vya Mali na vile vya Umoja wa Mataifa tangu mwaka 2011.
Wakati wanajeshi wengi wameuawa katika mashambulio madogo, pia wamekabiliwa kuwa mashambulio makubwa ambayo yamesababisha makumi wao kufariki, hasa wakati kambi zao nchini Mali zinaposhambuliwa.
Kisa cha kwanza ni kale cha – the “mauaji ya Aguelhok” January 2012, ambapo wanamgambo wa kijihadi wa Tuareg walipowaua wanajeshi 100 baada ya kuteka kambi moja ndogo katika eneo la jangwani.
Tukio hilo lilichangia kutoaminiana miongoni mwa maofisa wa kijeshi na matokeo yake yakawa uasi uliosababisha mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka huo.
Zaidi ya miaka saba baadae, licha ya mango wa muda mrefu wa muungano wa Ulaya kuwa na vikosi vya nchini humo ili kuwapa msaada na kutoamotisha bado majeshi hayo yanakabiliwa na mashambulio ya mara kwa mara.
Mwaka jana kati ya Septemba 30 September na Oktoba mosi, hadi maofisa 85 wa kijeshi walifariki wakati wanamgambo wa ISGS waliposhambulia kambi ya Boulikessi katika mpaka wa Burkina Faso.
Na baadae mwezi Novemba mosi 2019, wanajeshi wengine 49 waliuawa na wanamgambo wa ISGS walioshambulia kambi ya Indélimane, karibu na mpaka wa Niger mashariki mwa nchi hiyo.
Kipigo cha wanajeshi wa taifa hilo kutoka kwa makundi yenye itikadi kali inaelezwa kinatokana na ukosefu wa vifaa na mafunzo ya kijeshi.

Lakini pia inasemekana kuchangiwa na ukosefu wa uongozi mzuri wa kisiasa kutoka kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Baubacar Keïta hali ya kujihisi kutelekezwa na serikali ambayo ilisababisha kuchelewa kusainiwa kwa mkataba wa amani wa mwaka 2015 uliofikiwa kati ya serikali na wanamgambo wa kaskazini Tuareg wanaotaka kujitenga.
Kuchelewesha harakati za kuvunja nguvu za wapiganaji wanaotaka kujitenga na kun’gatua madaraka na fedha hadi katika ngazi ya kimaeneo imechochea hali ya kukata tamaa ambayo inaweza kuendeleza ugaidi.
Hali hiyo imekuwa chanzo kikubwa cha mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18 mwaka huu, ambayo viongozi wake walikuwa maofisa kadhaa walio na ujuzi na wanaofahamu mazingira magumu yanayowakabili wanajeshi katika eneo la kaskazini.
Katika kipindi kifupi kijacho, vikosi vya Mali vinaweza kuendelea na operesheni yao wakishirikiana na washirika wakuu wa kimataifa ambao wanajumuisha vikosi vya Ufaransa Barkhane, majeshi ya wanachama wenzao kutoka nchi tano za eneo la Sahel (Mali, Mauritania, Burkina Faso, Niger na Chad), kikosi kipya malum cha Muungano wa Ulaya kilichopelekwa sehemu ya Takuba pamoja na vikosi vya kulinda usalama vya Umoja wa Mataifa Minusma.
Jukumu la vikosi hivyo ni kudumisha ustawi wa nchi badala ya kuyatimua makundi ya kijihadi, lakini hatua hiyo haijasaidia kudhibiti usalama katika opareshini hiyo hatari duniani kwa Umoja wa Mataifa, ikizingatiwa kuwa wanajeshi 220 wameuawa tangu walipopelekwa huko 2013.
Lakini changamoto kuu inayokabili vikosi hivi vyote, vya kikanda na kitaifa ni kurudisha hali ya utulivu katika maeneo ya kaskazini na kati ya Mali na kukabiliana na makundi ya wanamgambo.
Barkhane kwa mfano imefanya msururu wa mashambulio dhidi ya makundi ya kijihadi, ambapo makamanda kadhaa wakuu wanaojulikana, akiwemo Abdelmalek Droukdel, kiongozi wa al-Qaeda Juni 3 mwaka huu alipoingia nchini Mali kutoka kaskazini mwa Algeria.
Lakini mashambulio kama hayo yamechangia kuongezeka kwa uhasama kati ya wapiganaji wa kijihadi na vikosi vya usalama katika kanda nzima ya kaskazini, kuanzia maeneo ya mto Niger na delta upande wa ndani karibu na Mauritania hadi mpaka wa mashariki ya mbali wa Niger.