NA NASRA MANZI

MASHABIKI wanaoangalia na kufuatilia mashindano ya Yamle Yamle Cup wamewaomba viongozi pamoja na wadau wa soka kuyaimarisha mashindano hayo, kwa kutafutiwa udhamini ili kuendelea kuwa na hamasa zaidi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa mtanange kati ya timu ya Mazombi FC dhidi ya Uzini Kombaini,ambapo Mazombi walishinda mabao 2-0.

Mmoja wa Mashabiki hao Juma Ali alisema mashindano yamekuwa na hamasa kubwa kutokana na vijana wengi kujitokeza mjini na vijijni.

Alisema licha ya kuwa na hamasa lakini kumekuwa na baadhi ya timu kukosa vifaa vya michezo,jambo ambalo huleta shida kwa timu hizo.

Aidha alisema mashindano hayo yamekuwa yakiwapatia fursa vijana kwa kusajiliwa katika timu kubwa,hivyo ni vyema kuimraishwa  .