BERLIN,UJERUMANI

MAWAZIRI wa fedha wa nchi za Umoja wa Ulaya watakutana mjini Berlin wiki ijayo,kujadili utekelezaji wa mpango wa ufufuaji uchumi wa euro bilioni 750.

Waziri wa fedha wa Ujerumani Olaf Scholz,alisema nchi za Umoja wa Ulaya zinapaswa kutumia fursa na rasilmali zake kufanya mageuzi kwenye uchumi wa nchi hizo.

Waziri wa fedha wa Ujerumani alisema ili kuurejesha uchumi wa Ulaya kwenye mkondo sahihi,ni muhimu kuwekeza kuungana na mageuzi yanayoaminika, ili uchumi wa mataifa hayo kuwa thabiti.