NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya Mayangi imefanikiwa kuwa bingwa wa mashindano ya kuwania Mbuzi baada ya kuichapa timu ya Parisi fc  mabao 4-2 ya penalti.

Fainali hiyo ilitimua vumbi uwanja wa Parisi Mahonda majira ya saa 10:00 jioni ambao ulikuwa na ushindani mkubwa,huku mashabiki wakijaa uwanjani.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumzikoni hakuna alifanikiwa kuzivaa vyavu za mwenzake.

Kurudi uwanjani kumalizia mchezo huo timu zilingia na kufanya mabadiliko,kila mmoja kutaka ushindi na kuwa bingwa,lakini dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliofanikiwa kupata bao.

Kutokana na matokeo hayo muamuzi wa mchezo huo aliamuru mikwaju ya penanti,ili kupatikana bingwa wa mashindano hayo na kukabidhiwa kombe.

Lakini ilionekana bahati kwenda kwa timu ya Mayangi ilipiga mikwaju hiyo na kukushinda minne,huku Parisi kushinda mikwaju miwili ambapo kombe la Mbuzi na mchele kilo 25 zilikwenda kwa Mayangi,huku Parisi wakijipatia Mbuzi mmoja.