PARIS, Ufaransa
MCHEZAJI wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou yuko kwenye maandalizi ya kuwa mjasiriamali baada ya kustaafu soka.
Hii ni baada ya mcheza soka huyo kupata shahada yake katika masuala ya Biashara kutoka Taasisi ya Biashara ya Lyon katika hafla iliyohudhuriwa na jamaa na marafiki siku ya Jumamosi, Septemba 12, kutoka kwa Chuo cha taaluma ya Biashara ya Lyon.
Nguli huyo alikabithiwa shahada hiyo baada ya kumaliza miaka mitatu ya masomo. Kalou alisaidia Cote d’Ivoire kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2015 kwa mara ya pili.