TOKYO, Japan

MSHAMBULIAJI wa Harambee Stars ya Kenya Michael Olunga ambaye anachezea timu ya Kashiwa Reysol ya Japan, alifunga bao la kufutia machozi wakati timu yake ilipofungwa bao 2 – 1 na Sagan Tosu katika mechi ya Ligi Kuu ya Japan iliyochewa hapo juzi.

 Olinga kwa sasa anaongoza msimamo wa wafungaji bora wa Ligi hiyo kwa magoli 16 baada ya kucheza mechi 15.

Bao lake dhidi ya Tosu lilipatikana katika dakika ya 24. Ushawishi wa Olunga unazidi katika kambi ya Reysol tangu aongoze kikosi hicho kupanda ngazi na kufikia Ligi Kuu mwishoni mwa msimu uliopita.

Katika mchuano wa mwisho ulioshuhudia Reysol wakiwapiga Gamba Osaka 3-0 , Olunga alipachika wavuni bao la kwanza katika dakika ya pili na kufikisha jumla ya magoli 15 kapuni mwake.