NA MWAJUMA JUMA

MCHEZO kati ya timu ya African Magic na Clickers wa ligi Kuu ya Zanzibar ya mpira wa Kikapu umeshindwa kumalizika baada ya kuingia kiza.

Mchezo huo ulichezwa juzi kwenye viwanja vya Mao Zedong na kuonesha ushindani mkali uliopelekea kumalizika kwa sare ya kufungana pointi 76-76, na kulazimika kuongezwa dakika tano ambazo zilishindwa kumalizika baada ya  giza kuingia.

Katika mchezo huo miamba hiyo ilionyesha ushindani mkali huku kila mmoja akishindwa kuamini , kwani imezoeleka timu za Pemba kushindwa kufanya vyema na kutoa ushindani.

Clickers mchezo wake kwanza waliwafunga ndugu zao wa California pointi 110-61 na mchezo wa pili walifungwa na Stone Town pointi 101-68 katika mchezo huo wa tatu walipambana kuhakikisha wanataka kuondoka na ushindi na kupelekea mchezo huo kuwa mgumu.

Miamba hiyo katika robo ya kwanza walimaliza kwa African Magic kuongoza kwa pointi 15-13, ya pili waliongoza tena kwa pointi 36-31 na ya tatu wakapata pointi 56 na Clickers pointi 51.