COLOMBO, SRI LANKA

MELI ya mafuta imeripuka jana katika bahari ya pwani ya mashariki mwa Sri Lanka na kuua mfanyakazi mmoja na wengine kujeruhiwa.

Taarifa zilisema kuwa meli hiyo ya mafuta ilibeba tani milioni 2.7 za mafuta yaliyokuwa yakisafishwa ikiendelea kuwaka kwa zaidi ya masaa 24 katika bahari za pwani ya mashariki mwa Sri Lanka.

Kwa mujibu wa jeshi la majini lilisema kuwa meli hiyo ya MT New Diamond ilikuwa ikielekea Bandari ya Paradip nchini India ikiwa imebeba mafuta yasiyosafishwa kutoka Kuwait wakati moto ulipotokea hapo jana asubuhi.

Msemaji wa Jeshi la Wanamaji, Indika de Silva aliambia Xinhua kwamba mfanyakazi mmoja ambaye alikuwa ndani ya chumba cha injini ambapo moto ulizuka alidhaniwa amekufa wakati mwingine aliyepata majeraha mabaya alikuwa ameokolewa na kuhamishiwa hospitali ya Kalmunai mashariki mwa nchi hiyo.

Wafanyakazi 22 waliosalia pamoja na nahodha na mhandisi wa chombo walikuwa wameokolewa na jeshi la wanamaji.

Indika alisema kuwa kufikia adhuhuri, jeshi la wanamaji lilikuwa likijaribu kusogeza meli ndani ya bahari ya kina kirefu huko Sri Lanka huku wakijaribu kuzima moto.

Meli mbili za Urusi ambazo zilijiunga na jeshi la wanamaji la Sri Lanka katika juhudi za uokoaji zilikuwa zimeondoka Ijumaa asubuhi lakini kwa sasa meli mbili za majini za India znasaidiana na wanamaji wa Sri Lanka.

Mpaka Ijumaa adhuhuri, hakukuwa na tishio la kumwagika kwa mafuta kwani jeshi la wanamaji lilifanikiwa kuzima moto, lakini wanamazingira wameonya kwamba ikiwa kutakuwa na uvujaji itakuwa na athari mbaya.