BARCELONA, Hispania
NAHODHA na mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi anaongoza kwenye orodha ya wanasoka wanapata fedha kubwa duniani, kwa mujibu wa Jarida la Forbes.


Malipo ya mshambuliaji huyo raia wa Argentina, yanamfanya kuwa mwanasoka anayelipwa kitita cha fedha nyingi kuliko wachezaji wengine, akimuacha kwa mbali mpinzani wake wa karibu, Cristiano Ronaldo, anayeshika nafasi ya pili kwenye orodha hiyo.

Uchunguzi uliofanywa na Forbes umebaini, Messi anakusanya kiasi cha dola za Marekani milioni 126 kwa mwaka huku Ronaldo akiingiza dola milioni 117.
Washambuliaji wa mabingwa wa Ufaransa PSG, Neymar na Kylian Mbappe wanafuatia katika nafasi ya tatu na ya nne.

Orodha kamili ya wanasoka wanakusanya fedha nyingi kwa mwaka, kwa mujibu wa Jarida la Forbes ni Lionel Messi (Barcelona na Argentina) $126m (£97.2m), Cristiano Ronaldo (Juventus na Ureno) $117m (£90.3m), Neymar (Paris St-Germain na Brazil) $96m (£74.1m) na Kylian Mbappe (Paris St-Germain na Ufaransa) $42m (£32.4m).

Wengine ni Mohamed Salah (Liverpool na Misri) $37m (£28.5m), Paul Pogba (Manchester United na Ufaransa) $34m (£26.2m), Antoine Griezmann (Barcelona na Ufaransa) $33m (£25.5m), Gareth Bale (Real Madrid na Wales) $29m (£22.4m), Robert Lewandowski (Bayern Munich na Poland) $28m (£21.6m)
na David de Gea (Manchester United na Hispania) £27m (£20.8m).(Goal).