LIONEL MESSI sasa anaweza kusajili jina lake kama nembo baada kushinda mzozo wa kisheria wa miaka tisa, mahakama ya juu barani Ulaya imeamua.

Mahakama ya haki ya Ulaya imetupilia mbali rufaa ya kampuni ya baisikeli ya Massi Uhispania na ofisi ya haki miliki ya muungano wa Ulaya, EUIPO.

Mchezaji soka huyo wa Barcelona alitoa ombi la kutaka kutumia jina lake kama nembo ya vazi la michezo mwaka 2011.

Lakini Massi alipinga ombi hilo likisema kuwa nembo hizo mbili zinakaribiana na huenda ikaleta mkanganyiko.

Mahakama ya Ulaya ya Haki (ECJ) imesema hadhi ya mchezaji nyota huyo itazingatiwa kutathmini ikiwa watu wataweza kutofautisha nembo hizo mbili.

Kwa kuzingatia hilo, ilidumisha uamuzi uliotolewa 2018 na mahakama ya pamoja ya EU ikisema mchezaji huyo anajulika vyema na kwamba suala la mchanganyiko haliwezi kutokea .

Massi, ambayo inauza baisikeli na vifaa vyake, ilifanikiwa katika hatua y akwanza ya kupinga ombi la mshambuliaji huyo wa Barcelona. Lakini ilishindwa baada ya Lionel Messi kuwasilisha rufaa katika mahakama ya Ulaya, ambayo imetoa uamuzi wa sasa.

Mnamo mwezi Agosti, mchezaji huyo aligongwa vichwa vya habari baada ya kuwasilisha ombi la kutaka kuondoka klabu ya Barcelona .

Barcelona na ligi ya La Liga zilisisitiza kwamba sheria hiyo ni sharti ifuatwe na kwamba klabu yoyote ambayo inataka kumnunua nyota huyo italazimika kulipa pauni milioni 624. Na Messi akalazimika kurudi katika mazoezi baada ya kusema kwamba hataishtaki klabu hiyo.