ULIMWENGU wa mataifa ya kiarabu umejikutaka kwenye mgawanyiko mkubwa hasa baada ya siku za hivi karibuni Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kutangaza kuanzisha uhusiano na taifa la kiyahudi la Israel.

Kuanzishwa uhusiano baina ya Umoja wa Falme za Kiarabu na Israel kumetokana changizo kubwa la Marekani ambayo imempa kazi ya kuisafisha Israel mbele ya mataifa ya kiarabu wazi wake wa mambo ya nje Mike Pompeo.

Makubaliano hayo, ambayo yameratibiwa na utawala wa rais wa Marekani Donald Trump, yanaufanya Umoja wa Falme za Kiarabu kuwa taifa la kwanza la kiarabu katika kipindi cha karibu miaka 26, kulitambua taifa la la Israel.

Kwa sasa Pompeo amekamilisha dili baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu kukubali kuwa na uhusiano na Israel, huku akiendelea na kazi ya kuyashiwi mataifa mengine katika ukanda wa mashariki ya kati wakubali kuanzisha uhusinao na Israel.

Pompeo anatumia gia ya kuziambia nchi za mashariki ya kati kwamba adui yao katika eneo hilo sio uwepo wa taifa la Israel, bali adui mkubwa katika eneo hilo ni taifa la kiislam la Iran.

Iran inachukuliwa na Marekani kama adui mkubwa katika eneo la mashariki ya kati hasa kutoka na sera zake kueleza wazi kuwa inapinga moja kwa moja uwepo wa taifa la Israel katika eneo hilo.

Makubaliano yaliyofikiwa baina ya UAE na Israel baadhi ya nchi zimepongeza, lakini baadhi ya nchi zimelaani kwa kile ilichokieleza kuwa ni kuisaliti Palestina ambayo ardhi yake kwa asilimia kubwa imeporwa na Israel.

Miongoni mwa nchi zilizoipinga UAE kuwa na mahusiano na Israel ni Uturuki ambayo ilisema historia na dhamira ya watu wa kanda ya mashariki ya kati havitasahau na wala kusamehe kile ilichokiita kitendo cha unafiki kilichofanywa na UAE.

Taarifa hiyo ya Uuruki iliongeza kwamba Umoja wa Falme za Kiarabu umefanya hivyo kwa maslahi yake finyu ili kuunga mkono mpango batili wa Marekani.

Kwa upande wizara ya mambo ya nje ya Iran, ilisema kilichofikiwa baina ya UAE na Israel ni upumbavu na kwamba mkakati huo utaimarisha upinzani dhidi ya Israel katika eneo la mashariki ya kati.

Iran ilisema UAE iliwadanganya watu wa Palestina kwa uamuzi huo wa aibu, haramu na wa hatari wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel na kuongeza kuwa wapalestina hawata wasamehe kwa makubali hayo.

Wapalestina wamelaani tangazo la makubaliano hayo na kumuita nyumbani balozi wao wa Umoja wa Falme za Kiarabu, ambapo hofu ya Palestina ni kwamba ndoto yake ya kurejeshwa kwa ardhi zake zilizoporwa na Israel na kuwa na taifa kamili inaweza isitimie.

Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas aliitisha mkutano uliozishirikisha pande zinazopingana kuweka msimamo mmoja dhidi ya makubaliano ya kuwepo uhusiano wa kawaida kati ya Israel na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Katika mkutano huo, Abbas alisema kwamba hawatamruhusu mtu yeyote kuwazungumzia na hawatairuhusu Marekanikuwa mpatanishi katika mazungumzo na Israeli na pia hawatakubali mpango wake wa makubaliano ya amani huku akitoa wito wa umoja wa wapalestina wakati huu wa mpango huo wa Marekani.

Abbas alikataa kushirikiana na serikali ya Trump kwa zaidi ya miaka miwili sasa akiishtumu kwa kuipendelea Israeli na pia kukataa mpango wa Trump kwa Mashariki ya Kati uliozinduliwa mwezi Januari mwaka huu.

Lakini taifa kubwa katika ulimwengu wa nchi za kiarabu na lenye ushawishi mkubwa Saudi Arabia linasemaje kuhusiano na baina ya UAE na Israel.

Hivi karibuni mfalme wa Saudi Arabia, Salman aliueleza msimamo wa taifa hilo kuhusiana na mahusiano baina ya UAE na Palestina pale alipozungumza kwa simu na rais wa Marekani, Donald Trump.

Katika mazungumzo yao, mfalma Salman alimueleza Trump kwamba dhamira ya Saudi Arabia ni kufikiwa makubaliano ya kudumu yatakayohakikisha uwepo wa taifa uhuru la Palestina.

Mfalme Salman alisema hilo ni sehemu kuu ya kuanzia ya juhudi za pendekezo la amani la mataifa za kiarabu na kwamba suala hilo linapaswa kutekelezwa.

Viongozi hao walizungumza kwa simu kufuatia makubaliano ya kihistoria yaliyosimamiwa na Marekani mwezi uliopita ambayo Umoja wa Falme za Kiarabu ulikubali kuwa taifa la tatu la Kiarabu  kurejesha  uhusiano  wa kawaida  na  Israel baada  ya Misri na  Jordan.

Mfalme Salman alimwambia Trump anakubaliana na juhudi za Marekani za kuunga mkono amani  na  kwamba  Saudi Arabia inataka  kuona  suluhisho la kudumu  na  la  haki  katika  suala  hili  la Palestina chini  ya  juhudi  za  amani  za  mataifa  ya  Kiarabu zilizopendekezwa  na  taifa  hilo  mwaka  2002.

Chini ya pendekezo hilo, mataifa ya Kiarabu yamependekeza kwa Israel kurejesha uhusiano wa kawaida ili kuweza kufikiwa makubaliano ya kupatiwa Wapalestina taifa lao na Israel kujitoa kabisa kutoka katika ardhi za mataifa ya Kiarabu ilizoziteka katika vita vya mwaka 1967 vya mashariki ya kati.

Saudi Arabia, mahali inapoaminika kuwa ndipo chimbuko na palipozaliwa dini ya kiislamu likiwa na maeneo matakatifu, hadi sasa haitambui Israel.

Hata hivyo, mwezi huu taifa hilo la Kifalme limesema litaruhusu safari za ndege kati ya Umoja wa Falme za Kiarbu na Israel, ikiwa ni pamoja na shirika hilo la ndege la Israel kutumia anga yake.

Mshauri wa ikulu ya Marekani na mkwe wa kiume wa Trump Jared Kushner alisema ana matumaini mataifa mengine ya Kiarabu yatarejesha uhusiano wa kawaida na Israel.

Hakuna taifa jengine la kiarabu lililosema hadi sasa kwamba linatafakari kufuata mfano wa Umoja wa Falme za Kiarabu kurejesha uhusiano na Israel.

Mtoto wa kiume wa mfalme Salman, mwana mfalme mteule Mohammed bin Salman na Kushner walijadili haja ya Wapalestina na Waisrael kurejea katika majadiliano na kufikia makubaliano ya kudumu ya amani.