NA MWAJUMA JUMA

TIMU ya soka ya Mfenesini A imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Baraza la Vijana kwa ushindi wa penalt 4-3 dhidi ya Mtopepo  B.

Mchezo huo ulichezwa kwenye kiwanja cha Dole majira ya saa 10:00 za jioni.Miamba hiyo ililazimika kupigiana mikwaju ya penalti baada ya kumaliza dakika 90 kwa kutofungana.

Kwa matokeo hayo timu ya Mfenesini A itakutana na timu ya Welezo katika mchezo wa fainali ambayo itachezwa Septemba 13.

Mbali na soka pia kwa upande wa mchezo wa nage, timu ya Six center na Welezo city wametinga fainali ya mchezo huo ambao ulikuwa ukishirikisha timu tano.

 Six Center imefikia hatua hiyo kwa kushika nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 12 na Welezo City imeshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi tisa.