NA BAKAR MUSSA

MGOMBEA wa uwakilishi kwa  tiketi ya ACT-Wazalendo jimbo la Mkoani, Seif Khamis Mohammed amesema, endapo wananchi wa jimbo hilo watamchagua atahakikisha wananchi wanafaidika na fursa za ajira.

Alisema hayo katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kunadi sera zake uliofanyika katika viwanja vya kwa Changaawe Mkoani.Alisema ni wajibu wake kuhakikisha ajira zinazotokea katika nafasi mbali mbali, zinawanufaisha wananchi wakiwemo wa Mkoani.

“Nawaahidi mkinichagua nitahakikisha nasimama kidete ili fursa zilizopo zitunufaishe sote badala ya wachache,” alisema.