NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa kikosi cha Coastal Union, Juma Mgunda ameusifia uwezo wa mshambuliaji mpya wa Azam FC Prince Dube.

Dube ni miongoni mwa wachezaji ambao wamesajiliwa msimu huu na wanaonekana kuanza vizuri

Dube kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union alifanikiwa kucheka na nyavu za timu hiyo mara mbili.

Akizungumza na Zanzibar Leo katika Uwanja wa Azam  Complex uliopo Chamazi Mgunda alimsifu Dube kuwa ni mchezaji mzuri.

“Dube nimemuona, ni mchezaji mzuri sio kwa sababu katufunga hapana lakini hadi msimu ukiisha kila mtu atakuwa najua ubora wake’’ alisema.