LONDON, England
KLABU ya Arsenal imemsaini mlinda mlango wa Iceland, Runar Alex Runarsson kwam mkataba wa miaka minne akitokea Dijon ya Ufaransa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiunga na miamba hiyo ya Ligi Kuu ya England kama kifuniko cha Bernd Leno, kufuatia kuondoka kwa Emiliano Martinez aliyekwenda Aston Villa.

Runarsson alihamia na Dijon mwezi Julai mwaka 2018 na alicheza mechi 13 msimu uliopita.
“Nina furaha na ninajivunia, ni siku kubwa kwangu na familia yangu,” alisema. “Najua itakuwa kazi ngumu, lakini, niko tayari kufanya kila niwezalo kupata dakika nyingi iwezekanavyo.”

Meneja wa Arsenal, Mikel Arteta alisema: “Tunataka kuunda ushindani mzuri wa nafasi na tunatarajia kuona Alex akileta kina zaidi kwenye nafasi ya walinda milango”.
Runarsson alifanya kazi na kocha wa makipa wa Arsenal, Inaki Cana wakati wote walipokuwa FC Nordsjaelland.(BBC Sports).