MAENDELEO ya sayansi na teknolojia ya habari duniani yanayotokana na matumizi ya intaneti kwa kiasi kibwa yamerahisha upatikanaji wa mawasilino kiasi cha ulimwengu kuwa kama kijiji.

Tunakumbuka vyema kabla ya kuenea matumizi ya simu za mikononi, suala la mawasiliano likuwa gumu sana baina ya ndugu, jamaa na marafiki, lakini kukua kwa teknolojia changamoto hiyo imeondoka kabisa.

Enzi hizo kama umepata msiba kijijini, wahusika wa msiba huo walilazimika kutafuta usafiri wa baiskeli ama gari za alfajiri yenye ruti moja kwenda na kurudi mjini kuwaarifu ndugu na jamaa kuhusu msiba.

Aidha wazee wetu hivi sasa wakati wa ujana wao walivyokuwa na nguvu za kutosha walilazimika kutumia baiskeli kwenda na kurudi mjini kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu kwa ndugu na jamaa.

Changamoto hiyo imeondoka kwani hivi sasa huna haja ya kulala garini kwenda na kurudi mjini kutoka kijiji chochote gari zipo hadi usiku, kitu cha muhimu ni ratiba yako.

Lakini kama huoni sababu ya kwenda mjini kutoa taarifa yoyote uliyonayo basi vuta simu yako ta mkononi mpigie kila mtu na umuarifu taarifa yako kwa wakati huo huo ujumbe utakuwa umefika.

Maendeleo ya simu za mikononi hayaishii kupiga na kupokea simu kwa ajili ya kupeana taraifa na habari, kwani simu hizo zinawezesha kufanyakazi nyingi kwa wakati mmoja.

Simu ya mkononi hivi sasa inaweza ikatumika kama redio, kama televisheni, kama tochi, inaweza kupiga kuisanifu na kurusha picha za video na picha za kawaida nakadhalika.

Kwa kutumia intaneti simu hizo pia inawezesha kutuma habari kwa njia za mitandao ya kijamii kama whatsup, twitter, Instagram, you tube, WeChat, facebook na kadhalika.

Kwa hakika waliobuni na kutuletea simu za mikononi walifanya jambo jema sana la kuturahisisha mawasiliano baina yetu, lakini kitu cha kushangaza sana mitandao ya kjjamii inayapatikana kwenye simu inatumika kinyume na makusudio.