NA MWANDISHI WETU
MJUMBE wa NEC ya Chama cha Mapinduzi, Mwita Haji Ali, amemtaka Naibu Kiongozi wa ACT Wazalendo, Juma Duni Haji kutaja sera za chama chake , kwa kuhimiza ustawi wa umoja , Amani na kuacha siasa za kubaguzi.
Amemueleza hakuna kigezo kwa mgombea urais lazima achaguliwa Mtwara, Pemba Kaskazini , Unguja Kusini au Mwanza kama anavyodai wagombea wa CCM Zanzibar huchaguliwa Dodoma.
Hayo yametamkwa jana huko Makunduchi na Mjumbe huyo ambaye alisema hoja hiyo haina msingi kuwaaminisha wananchi kwani hata Mgombea Urais wa ACT Wazalendo Maalim Seif toka tokea mwaka 1995 amekuwa akichaguliwa jijini Dar es Salaam.
Mwita alisema Duni anekosa werevu pia hama ubavu na uwezo wa kubadili lolote lilipangwa na CCM, na madai anayoyatoa katika kampeni zake hayana ukweli kwa kudai Zanzibar imemezwa na anawapotosha wananchi.
“Duni ajenge hoja na kutaja sera za ACT Wazalendo aache porojo na kulialia majukwani tokea mwaka 1995 hata chama chao huitisha mikutano Tanzania Bara hata mwaka huu wagombea wao wamepitishwa mlimani City kwanini aishangae CCM vikao vyake kuitisha Dodoma” Alihoji Mwita.