NA ABOUD MAHMOUD

CHAMA cha Mpira wa Ukuta Zanzibar (ZSRA) kimesema mara baada ya kumaliza ujenzi wa uwanja wao, wamejipanga kwenda kwenye skuli mbali mbali kutoa elimu ya mchezo huo kwa walimu na wanafunzi.

Akizungumza na Zanzibarleo, Katibu wa chama hicho Mohammed Hamza alisema kutokana na kuwepo kwa viwanja kidogo, hivi sasa ni vigumu kutoa elimu lakini mara baada ya kumaliza kwa ujenzi huo wataweza kutoa elimu.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kupata wachezaji wengi na kuutangaza mchezo huo pamoja na nchi kwa ujumla kitaifa na kimataifa kama ilivyo nchi nyengine.

“Hivi sasa watoto wanaocheza mchezo huu ni watoto wetu wenyewe ambao tunawachukua mazoezi, ndio maana tukaamua tukimaliza ujenzi wa uwanja mpya wa Maisara tutapita skuli kutoa elimu ili iweze kufahamika na kupata wachezaji wengi,”alisema .