NA MWANAJUMA MMANGA

BENEDECTED Dominic Masawe (26) mkaazi wa Mkaazi wa Dar-es-Salaam, amefariki dunia baada ya kuzama wakati akiogelea  katika hoteli ya Water Front iliyoko Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman, alisema tukio hilo limetokea Agosti 29 mwaka huu majira ya saa 23 :00 huko hoteli ya Water Front na marehemu huyo aliondoka kwao Tanzania bara kwa lengo la kuja Zanzibar, kwa ajili ya utalii wa ndani ndipo alipofika katika hoteli ya Water Front aliamua kuogelea na kuzama na hatimae kufariki duinia.

Alisema chanzo cha kifo chake marehemu huyo, alikunywa maji na kushidwa kupumua hadi mauiti hayo yalipomfika na marehemu huyo alichukuliwa na watu wa hoteli na kupelekwa katika hospitali ya Mnazi mmoja kwa ajili ya uchunguzi na kubainika alikunywa maji na kuzidiwa.

Alisema marehemu huyo baada ya kubainika amehifadhiwa Hospitali ya Mnazimmoja, ili kusubiri  jamaa zake kusafirishwa kwa mazishi na ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari pale wanapoogelea kuwa waangalifu na badala yake kuangalia kima cha maji ili kuepusha maafa wakati yanapotokezea.

Wakati huo huo ajali ya gari kumgonga mwenda kwa miguu na kusababisha majeruhi. Huko Kidimni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Akithibitisha kamanda wa mkoa huo Suleiman Hassan Suleiman alimtaja aliegongwa na Nassor Juma Kabula (7) mkaazi wa Kidimni ambae ni mwanafunzi wa skuli ya Kidimni na tukio hilo limetokea majira ya saa 15: 10 huko Kidimni Wilaya ya kati.

Suleiman akielezea chanzo cha ajail hiyo alisema kijana huyo Nassor alikuwa anarudi skuli ndipo ikatokea gari yenye namba za usajili Z.803 CH aina ya Kanta ikitokea Koani na kuelekea Kidimni na kutokea mwanafunzi huyo akikata njia na hatimae kumgongwa kusababisha kumuumiza mguu na sehemu zake mbali mbali za mwili.

Alisema baada ya kugongwa mwanafubnzi hyo na kuchukuliwa na kupelekwa hospitali ya mnazi mmoja kwa ajili ya kupatiwa matinbabu na hali yake inaendelea vizuri.

Hivyo Kamanda Suleiman alitoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wakati wanapokuwa barabarani kupunguza mwendo kasi,  ili kuepusha ajali zisizokuwa za ulazima.