NA NASRA MANZI

MASHINDANO ya Yamleyamle  cup yanazidi kutimua vumbi kwa kupigwa michezo mbali mbali katika viwanja viwili.

Mchezo wa kwanza uliowakutanisha timu ya Magari ya mchanga dhidi ya Mtende City ,uliopigwa  katika uwanja wa Magirisi Taveta.

Katika pambano hilo timu ya Magari ya mchanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwa bao 1-0.Bao pekee la ushindi liliwekwa wavuni na Said Mwinyi katika dakika ya 44.

 Wakati dimba la Ziwani Polisi kulipigwa mchezo kati ya timu ya Kijuuni dhidi ya FC timu yetu.Katika pambano hilo FC timu yetu ilifanikiwa kuibuka na ushindi kwa magoli 3-1.

Magoli ya washindi yaliwekwa kimiani na Sadala Mohamed dakika ya 21-34 ,wakati bao la mwisho lilifungwa na Ayoub Kaheke mnamo dakika ya 43.

Huku bao pekee la kufutia machozi la timu ya Kijuuni likifungwa na mchezaji Ibrahim Khamis kwenye dakika ya 32.