NA MARYAM HASSAN

MSHITAKIWA   Ali Hamad (54) mkaazi wa Mboriborini ameiomba mahakama kumpa muda wa kwenda hospitali kwa sababu bado anaumwa.

Mshitakiwa huyo alitoa ombi hilo mbele ya Hakimu Hamisuu Saaduni Makanjira, baada ya upande wa mashitaka kudai kuwa shahidi hawajapatikana.

Alisema bado anasumbuliwa na maumivu makali hivyo aliiomba mahakama kumpa muda zaidi ili azidi kufanya uchunguzi kwa matatizo yanayomsumbua.

Huku upande wa mashitaka iliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Hariri Yoshau alisema kuwa hawajapokea shahidi katika kesi hiyo.

Hivyo aliiomba mahakama kuahirisha shauri hilo na kupanga tarehe nyengine kwa ajili ya kusikiliza ushahidi huku wakizingatia ombi alilotoa mshitakiwa.

Baada ya kutoa maelezo na ombi hilo kuwasilishwa mahakamani Hakimu wa mahakama hiyo aliahirisha shauri hilo na kupangwa kusikilizwa tena ushahidi Novemba 11 mwaka huu.

Khamis ambae alifikishwa mahakamani hapo kwa kosa la shambulio la aibu alilodaiwa kutenda mnamo mwezi wa Agosi mwaka 2018 siku tofautii majira ya 2:00 za asubuhi.