KAMPALA,UGANDA

RAIS wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ameelezea kuunga mkono kwake katika kuongeza ufadhili wa mipango muhimu inayokusudiwa kuinua wanawake na vijana walio katika mazingira magumu ya  umaskini.

Aliyasema hayo katika hafla kukabidhi vifaa vya kisasa vya kuanzisha biashara walivyokabidhiwa vijana na wanawake 3,228 ambao walipangwa katika vikundi 190 katika mkoa mdogo wa Busoga.

Museveni alisema kuwa Kadaga ana haki ya kutaka pesa zaidi ziingizwe katika programu ambazo zinaondoa umaskini badala ya kupata pesa za kuongeza mishahara ya wafanyakazi wa umma.

“Asante Waganda kwa kukumbuka vitu vinavyotengeneza pesa na Kila mtu sasa ana hamu ya kushiriki katika kupata pesa. Ninafurahi kwamba Spika anasema tunaongeza pesa katika miradi hii ya kutokomeza umaskini,”Museveni alisema.

Alisema hapo awali,viongozi wengine walikuwa wakisema wanaweka  pesa katika mishahara na vitu vyengine, lakini sasa zinapaswa kuwekwa katika miundombinu na miradi ya kutokomeza umaskini.

Kadaga alitaja pesa hizo kuwa Shilingi 50 bilioni kwa Programu ya ajira ya Kijani, Shilingi bilioni 30 kwa mpango wa Kujitolea wa Kitaifa wa Wanafunzi na Wahitimu, Shilingi bilioni 30 kwa Mradi wa Uhamasishaji Kijani wa Uganda (UGIP) – Songhai Model, Kazi za Shilingi bilioni 100 kwa Vijana wa Mjini (JOY), Shilingi 20 bilioni kwa Upataji wa haki ya Kazi na Sh50 bilioni kwa kuboresha uzalishaji wa kazi.

Mpango wa ajira ya Kijani ni mpango mkakati wa Serikali wa kuunda ajira nzuri kwa kupunguza athari mbaya za mazingira na kukuza usalama na afya kazini unaosababisha biashara na uchumi endelevu wa mazingira.

Mradi wa Kuboresha Uzalishaji wa kazi na Ushindani unataka kuanzisha Kituo cha Uzalishaji cha Kitaifa ambacho kitaratibu na kuongoza uzalishaji,upimaji, utafiti na usambazaji.

Mpango wa Kujitolea wa Kitaifa wa Ufundishaji na Wahitimu unakusudia kujitolea kama njia muhimu kwa ukuzaji wa ujuzi wa vijana.

Mradi wa ajira kwa vijana wa mjini (JOY) unaongeza ajira na tija ya kazi ,Vikundi vilivyofaidika na kitengo cha pili kitaajiri moja kwa moja zaidi ya watu 5,000 na msaada ambao ulitolewa utaongeza tija na faida ya biashara hizo kwa kuongeza ukuaji wa biashara na kuchangia katika kuunda ajira.

Kukabidhi vifaa vya kuanzisha biashara kwa vikundi ni juhudi kubwa na Serikali kusaidia vijana na wanawake kupitia utoaji wa teknolojia za kijani kibichi, mafunzo, udhibitisho na idhini.

Chini ya sehemu ya msaada kwa sekta isiyo rasmi, lengo ni kutoa vifaa vya kuanzisha biashara kwa wafanyabiashara 1,000,000 ili kuwanufaisha vijana, wanawake na Watu Wenye Ulemavu (PWDs).

Ili kukuza zaidi msaada kwa sekta isiyo rasmi,Serikali kupitia mpango wa ajira ya Kijani, ilipanga kuanzisha Makao ya Biashara ya Viwanda na Vituo vya Watumiaji wa Kawaida.