NA TATU MAKAME

HAMIDA Ramadhani Juma (29) mkaazi wa Mwembeladu Wilaya ya Mjini Unguja, amepandishwa katika Kizimba cha Mahakama ya Mkoa Vuga baada ya kupatikana na dawa za kulevya.

Mwanadada huyo alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa kosa lake na Mwendesha Mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Shamsi Yasin Saada mbele ya hakimu Salum Hassan.

Kosa hilo alilitenda Septemba 17, mwaka 2017, mnamo majira ya saa 4:30 za asubuhi jambo ambalo ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 15 (1) (a) cha sheria ya kudhibiti dawa za kulevya sheria namba 9 ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho chini ya  kifungu cha 11 (a) cha sheria namba 12 ya mwaka 2011.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo mshitakiwa huyo alipatikana na dawa za kulevya mfumo wa unga aina ya heroin wenye uzito wa grams 22.58.

Hata hivyo, kesi ya mshitakiwa huyo itasomwa tena jana mwaka huu, ambapo mshitakiwa huyo yupo rumande kutokana na kuwa kesi hiyo haina dhamana.