TBILISI, GEORGIA
JESHI la Georgia limekamilisha zoezi la kijeshi na Washirika wake huko kituo cha jeshi karibu na mji mkuu wa nchi hiyo.
Wizara ya Ulinzi ya Georgia alisema zoezi hilo limewashirikisha wanajeshi wapatao 2,700 kutoka nchi za Georgia, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Poland.
Mazoezi hayo ni pamoja na mafunzo ya utumiaji wa zana za moto, zana za wanaanga kama ndge, zana za baharini na nchi kavu.
Taarifa kutoka nchini humo zilisema kuwa mazoezi hayo yalianzishwa mwaka 2015, ambapo pamoja na mambo mengine yalilenga kuwapa mafunzo wanajeshi wa Georgia na kuboresha ushirikiano wa wanajeshi wa nchi washirika na vitengo vya Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO)