BERLIN,UJERUMANI

MAELFU  ya waomba hifadhi wamelala nje kwa usiku wa tatu kwenye kisiwa cha Lesbos baada ya kambi kubwa kabisa ya wahamiaji nchini Ugiriki kuteketea kwa moto.

Polisi walifika kwa wingi katika eneo hilo huku wengine wakiwazuia wahamiaji kufika katika bandari iliyo karibu.

Maofisa wa Ugiriki waliwalaumu wahamiaji kwa tukio hilo la moto katika kambi ya Moria, ambalo lilitokea baada ya watu 35 kupatikana na virusi vya corona na walikuwa chini ya vizuizi.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya ndani wa Ujerumani Horst Seehorfer alisema nchi kumi wanachama wa Umoja wa Ulaya walikubali kuwachukua karibu watoto wadogo 400 wasioandamana na mtu kutoka kambi hiyo iliyoungua. Ujerumani na Ufaransa zitachukua idadi