NA FATUMA KITIMA, DAR ES SALAAM

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha ACT –Wazalendo, Omar Said Shaaban, ameomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kupitia upya kuwatoa wagombea wa ubunge, uwakilishi na udiwani wa chama hicho katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu utaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Amesema ni vyema Tume hizo za NEC na ZEC wakapitia tena uamuzi wao juu ya rufaa zilizokatwa na wagombea wa chama cha ACT- Wazalendo, ili waweze kuwapitisha Wabunge, Wawakilishi na Madiwani.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini hapa jana, amesema chama cha ACT- Wazalendo pamoja na kufahamu sheria ya uchaguzi ya Zanzibar namba nne ya mwaka 2018, kifungu cha 54 na Tume ya Taifa ya uchaguzi kifungu cha 40 na  kifungu kidogo cha sita inaeleza maamuzi ya tume kwa rufaa zinazo uteuzi zinakuwa za mwisho.

Aidha alisema kwa wagombea wa Zanzibar Wabunge sita (6) rufaa zao zilikataliwa na tume kwa madai kuwa ziliwasilishwa nje ya muda, kwenye majimbo ya Wawi , Kiwani, Mbole, Mkoani ,Chambani na Kijini .

Aidha alisema ,wagombea wote wamewasilisha ndani ya muda masaa 24 kama inavyoelekezwa na kanuni ya 31 kanuni ndogo ya kwanza ya kanuni za uchaguzi wa Rais na Wabunge za mwaka 2020.

Alifafanua kuwa Chama kimejiridhisha kuwa mgombea wa jimbo la Wawi aliwasilisha rufaa yake na kupokelewa Agosti 28, mwaka huu, saa 11: 15 jioni ikiwa ni masaa 20 tangu kutoka uamuzi wa msimamizi wa uchaguzi juu ya pingamizi wa siri za uchaguzi ambao ulitolewa Agosti  27  mwaka huu, saa 3:30 usiku .

Aliongeza mgombea huyo aliwasilisha rufaa yake saa 11:00 jioni nakusema wanavielelezo vya fomu ya rufaa na muda ambao imepokelewa ,vilevile kuhusu ndivyo ilivyokuwa Jimbo la Ole, ambao uamuzi wa pingamizi umetoka 27 saa 3:00 Usiku na rufaa kupokelewa tarehe 28 jioni pamoja jimbo la Kiwani ambao uamuzi wa pingamizi ulitoleawa tarehe 28, na rufaa imepokelewa saa 2:00 asubuhi tarehe 28.

Pia alisema mgombea wa jimbo la Kijini akiwasilisha rufaa tarehe 28 saa 4:00 asubuhi kwakuwa uamuzi wa pingamizi umetolewa tarehe 27 ,nakudai kuwa taarifa zilizopelekwa sio saihi kwa tume ya taifa ya uchaguzi .