PARIS, Ufaransa

NYOTA wa klabu ya PSG, Neymar Jr alikuwa ni miongoni mwa nyota watano ambao walionyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Ligue 1 uliochezwa usiku wa kuamkia jana mbele ya Marseille wakati timu yake ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Bao la ushindi kwa Marseille lilipachikwa na Florian Thauvin dakika ya 31 na kuwafanya PSG kukosa pointi tatu kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Parc des Princes.

Kwa PSG, nyota watatu walionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+7 walikuwa wawili ambao ni Layvin Kurzawa ambaye alionekana akipigana na Jordan wa Marseille na Leandro Paredes naye alikutana na kisanga cha kadi nyekundu huku Neymar akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+7.

Wawili wa Marseille ni Jordan Amavi na Dario Benedetto nao ilikuwa dakika ya 90+7.

Mwamuzi wa kati, Jerome Brisard hakuwa na chaguo kwa kuwa nyota hao walionekana wakifanyiana ubabe ndani ya uwanja na Neymar yeye alionekana akizozana na beki, Alvaro Gonzalez pia anatajwa kufanya tabia ya ubaguzi wa rangi.