BARCELONA, Hispania
KLABU ya FC Barcelona wamekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji raia wa Bosnia na Herzegovina, Miralem Pjanic.

Pjanic amejiunga na miamba hiyo ya Ligi Kuu ya Hispania akitokea kwa mabingwa wa Italia, Juventus na amekabidhiwa jezi nambari 8, iliyoachwa na Arthur Melo na iliyokuwa ikivaliwa na kiungo, Andres Iniesta hapo awali.

Wakati huo, Barca wameripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi na Olympic Lyon ya Ufaransa, Memphis Depay, kwa dau la pauni milioni 26.
Kocha wa Barca Ronald Koeman, ambaye aliwahi kufanya kazi na mshambuliaji huyo alipokua kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, anatajwa kusukuma mpango wa kusajiliwa kwake.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, amekua na mafanikio makubwa tangu alipotua Olympic Lyon mwaka 2017, kwani hadi sasa ameshafunga magoli 57 katika michezo 139 akiwa na klabu hiyo inayoshiriki ‘Ligue 1’ ya Ufaransa.(Goal).