NA ASIA MWALIM
JESHI la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja limevitaka vikosi vya ulinzi shirikishi Mkoani humo kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kuilinda na kuitunza amani ilioopo nchini.
Kamanda wa polisi mkoa huo ACP, Awadh Juma Haji aliyasema hayo wakati wa kikao cha cha vikosi hivyo, huko ofisini kwake Mwembe Madema Zanzibar.
Kamanda Awadh alisema vikundi hivyo endapo watashirikiana na kuchukua hatua za kuendelea kuilinda amani hasa kwa wakati huu wa kufunguliwa kampeni sambamba na kuelekea uchaguzi mkuu ambapo wananchini hutegemea amani hiyo.
“Wananchini wa mkoa huu wanahitaji kufanya mambo yao wakiona amani imetawala hivyo hatutasita kuwalinda” alisema.
Aidha alivitaka vikundi hivyo kufuata sheria na muongozo waliowekewa sambamba na kujiepusha na watu wasioipenda amani na maendeleo ya nchi.
Alifahamisha kuwa lengo la kuanzishwa vikundi hivyo na kuwepo askari hao ni kupambana na vitendo vya kihalifu na wahalifu pamoja na vitendo vinavyo vuruga amani ndani ya mkoa huo.
Awadhi alivipongeza vikundi hivyo kwa kujitolea kufanya kazi hizo ambazo lengo lake ni kupambana na wale waliodhamiria kufanya uhalifu pamoja na vitendo vinavyopelekea kuvuruga amani ndani ya mkoa.
Aidha Kamda Awadhi alivitaka vikundi hivyo kuacha kutumika kama sehem ya kufanyia uhalifu kwani kumekuwa na baadhi yao ambao hushiriki kufanya uhalifu kwa kupitia vikundi hivyo.
“Kuna askari wanazitumia vibaya nafasi zao kwa kutumiwa na kushirikishwa kufanya fujo zinazohatarisha amani hatutamvumilia askari huyo” alisisistiza kamanda.
Hata hivyo, aliwataka wananchini wa mkoa huo kushirikiana katika kuilinda amani hivyo wasiache kutoa taarifa zinazoashiria uvunjifu wa amani kwa jeshi hilo.