MOSCOW,URUSI

POLISI  ya Urusi imesema kuwa inapanga kumuhoji kiongozi wa upinzani Alexei Navalny mjini Berlin, baada ya serikali ya Moscow kupuuza kauli ya Ujerumani kuwa alipewa sumu inayoathiri mishipa ya fahamu ya Novichok.

Polisi ya Urusi ilisema kufuatia ripoti kuwa Navalny alianza kupata fahamu, huenda watahitaji kumuuliza maswali ya ufafanuzi na ya ziada, na wawepo wakati wenzao wa Ujerumani wakiendelea na uchunguzi wao na Navalny, madaktari na watalaamu.

Serikali ya Urusi inapinga majaribio yoyote ya kuilaumu Urusi kwa tukio hilo la sumu, na inasema inataka kujua nini kilitokea.

Wanasiasa wa kimataifa wanasema tukio hilo linaloonekana kuamrishwa na Serikali na kuitaka Urusi ithibitishe kutohusika kwake. Mkosoaji huyo wa Serikali ya Urusi mwenye umri wa miaka 44 na mwanarakati wa kupambana na rushwa aliugua baada ya kupanda ndege katika mkoa wa Siberia na akalazwa huko kabla ya kusafirishwa Ujerumani.