WASHINGTON,MAREKANI

WAZIRI  wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo amelaani jaribio la Belarus inayokabiliwa na maandamano kuwafukuza kutoka nchini humo viongozi wa upinzani na kusema Marekani inatafakari kuiwekea nchi hiyo vikwazo zaidi.

Pompeo alisema Marekani inawasi wasi mkubwa kutokana na hatua siku ya Jumatatu dhidi ya Maria Kolesnikova, mmoja wa watu mashuhuri kabisa ambao bado wako ndani ya nchi hiyo, na alisifu ujasiri wake.

Alisema katika taarifa kuwa Marekani kwa ushirikiano na washirika wake, inatafakari kuweka vikwazo zaidi ili kuwawajibisha wake wanaohusika katika ukiukaji wa haki za binadamu na ukandamizaji nchini Belarus.