KINSHASA,DRC
RAIS wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefanya mkutano wa ghafla na mtangulizi wake Joseph Kabila katika kipindi ambacho maofisa katika Serikali tete ya muungano wakisema, kiongozi huyo wa zamani anaweza kurejea katika ulingo wa kisiasa.
Tshisekedi,ambae alichukua madaraka kutoka kwa Kabila Januari, mwaka uliopita,anaongoza sambamba na uungwajwaji mkono wa mtangulizi wake,ambae ana ufuwasi mkubwa bungeni na kushika karibu sehemu kubwa ya nyadhifa za kiserikali.
Taarifa iliyoandikwa katika ukurasa wa Twitter kutoka upande wa wabunge wa upande wa Kabila inaeleza viongozi hao wawili walijadiliana maendeleo ya muungano unaongoza serikali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP katika miezi ya hivi karibuni, bado kumekuwa vuta ni kuvute baina ya pande hizo mbili.
Hivi karibuni Waziri wa Mazingira, Claude Nyamugabo alisikika akisema alianza kufanyia kazi suala la Kabila kurejea katika kiti cha urais, ambao unatarajiwa kufanyika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Alisema Kabila ni rais wa chama chake na anaamini katika kurejea kwake madarakani.
Rais Kabila ambae alidumu madarakani kwa takribani miaka 18 alikuwa kimya katika kipindi kirefu na kwa kiasi kikubwa amekuwa akijiepusha kuonekana hadharani.