ADDIS ABABA, ETHIOPIA

RAIS wa Ethiopia Sahle Work Zewde alisifu Uwanja wa Urafiki uliojengwa na China,ambao uko katikati ya Addis Ababa, mji mkuu wa nchi hiyo.

Uwanja wa Urafiki ulijengwa na Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China (CCCC) ndani ya mwaka mmoja.

Rais Zewde alisema,waethiopia wote wanajivunia uwanja huo wa burudani ya umma unaendana na sifa ya Addis Ababa kama mji mkuu wa Afrika.

Mradi huo na mambo mengine yaliyofanywa yataongeza hadhi ya mji huo.

Balozi wa China nchini Ethiopia Tan Jian alisema Uwanja wa Urafiki ni zawadi iliyokuja kwa wakati kwa watu wa Ethiopia, ambao wanasherehekea Mwaka Mpya wa Ethiopia.