NA ZAINAB ATUPAE

TIMU ya Chumbuni imepokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu ya Real 9, ikiwa ni muendelezo wa mashindano ya Coco Sport Ndondo Cup hatua ya mtoano.

Mchezo huo uliotimua vumbi uwanja wa Kiembe Samaki majira ya saa 10:00

Mtanange huo uliokuwa wa ushindani kwa timu zote kila mmoja akisaka ushindi ili kuendelea hatua nyengine kwenye mashindano hayo.

Dakika ya Abdalla Seif wa timu ya Real 9 alifunga bao la kwanza katika dakika ya pili, ambalo lilidumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.

Kurudi uwanjani kumalizia kipindi cha pili timu zilingia kwa kufanya mabadiliko ambapo dakika ya 75 Haji Abrahman wa timu ya Chumbuni, alifunga bao la kufutia machozi,huku bao la ushindi la timu ya Real 9 lilifungwa na Ahmed Pisi dakika ya 87.

Katika mchezo huo mchezaji bora aliteuliwa Haji Abrahman wa timu ya Chumbuni.

Mchezo uliotarajiwa kupigwa juzi kati ya timu ya Machakosi na Wakoloni haukufanyika baada ya timu ya Machakosi kushindwa kufika uwanjani bila ya sababu.